TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 17 Februari 2015

JUMANNE ULAYA APATWA NA MALARIA GHAFLA MKOANI LINDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Mpiga gitaa wa kutegemewa wa Ogopa Kopa na mkuu wa nidhamu wa bendi hiyo Jumanne Ulaya, ameshikwa na maralia kali iliyoambatana na mafua makali wakati wakiwa katika ziara ya bendi hiyo iliyofanyika katika mikoa ya kusini yaani Lindi na Mtwara hivi karibuni.

JUMANNE ULAYA "J4".
       Akizungumza na mtandao huu J4 alisema alianza kujisikia kifua kizito sana na sauti kuanza kumkauka, hali iliyopelekea na kichwa kuanza kumuuma sana, hii ilinifanya nikimbilie hospitali na kugundulika kuwa nina maralia. kwa sasa natumia dawa na nimerejea Dar naendelea na matibabu.

        Kwa sasa hali ya hewa ya mikoa ya kusini ni tofauti sana na Dar kwahiyo kupatwa maradhi kwa msanii huyu ni kitu cha kawaida katika kubadili mandhali ya hali ya hewa, ubuyuwataarabutz.blogspot.com Unapenda kuchukuwa nafasi hii kukupa pole kwa maradhi hayo kikubwa endelea kutumia dozi utakaa sawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni