TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 3 Mei 2015

ASIA MARIAM:- SIJAONA THAMANI YA PENDO NI BORA KULIKO MAPENZI HAYANA DHAMANA WA ISHA MASHAUZI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Asia Mariam ni jina linalokuja kwa kasi kubwa sana katika tasnia hii ya taarab hapa nchini tanzania, huyu ni muimbaji wa Wakaliwao modern taradance na kwa sasa anatamba na wimbo wake uitwao "Sijaona thamani ya pendo".


ASIA UTAMU

            Siku ya jana jumamosi nilipata bahati ya kukutana nae pale katika ukumbi wa Lango la jiji magomeni mikumi katika show ya Gusagusa min bendi na nilitaka kujua mawili matatu toka kwake hususani juu ya hizi tuzo za Kili music award's ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele sana na wadau juu ya baadhi ya wasanii walioteuliwa kugombea kuonekana kwa wadau kwamba hawana vigezo!.


       Nilimuuliza Asia anachukuliaje tukio la kuonekana nyimbo yake ya Sijaona thamani ya pendo kutoingia katika kinyang'anyiro hicho cha Kili na badala yake wimbo wa Isha mashauzi uitwao Mapenzi hayana dhamana kuteuliwa kugombea kama wimbo bora wa mwaka?.


ASIA UTAMU.

    Mimi sikubaliani na hilo lililofanywa na hao wanaojiita wajumbe wa kamati hiyo ya kili music award's, wimbo wangu ni bora zaidi kuliko huo wimbo wa Isha mashauzi, kwa kutolea ushahidi, wimbo wangu umeshindanishwa na huo wimbo wa Isha zaidi ya redio 5 hapa nchini na nimekuwa nikimbwaga kwa kula nyingi sana tu!, labda kama wameamua kubebana kwa majina kama wafanyavyo miaka yote sawa haina shida, ila wajue wazi kwamba wanatuvunja nguvu sisi wasanii tunaochipukia!.


      Ina maana kila mwaka wanaojua ni hao hao tu?, Au kama kuna kamchezo huwa kanafanywa humo kwenye kamati yenu kuweni wawazi tu ili kila mwaka mshiriki pekee yenu! maana tumechoka kuwa wasindikizaji alimalizia kwa kusema Asia mariam!.


       Asia Mariam amekuwa ni miongoni mwa wasanii lukuki ambao wamekuwa wakiendelea kushusha tuhuma nzito kwa waandaaji wa tuzo hizi za kilimanjaro music award's wakionyesha kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanywa katika kamati husika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni