NA KAIS MUSSA KAIS.
Asalaam aleykum wasomaji wangu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com, natumai mpo vizuri sana, leo tunakutana tena hapa hapa kijiweni kwetu tupige stori kidogo kuhusu hizi tuzo za kilimanjaro music award's.
Utaratibu uliowekwa na kamati ya kilimanjaro music award's mwaka huu wa kumpigia kura kwa kumteua msanii aingie katika mpambano ndio chanzo cha malalamiko yanayo endelea toka kwa wadau wa muziki huu hapa nchini. Unapomwambia mtanzania kwamba anachotakiwa kufanya ni kupiga kura kwa simu ili kumpendekeza msanii umpendae ni sawa na kumsukuma mlevi...maana hupati shida!.
Kipengele cha kwanza ambacho wadau wamekuwa wakikilamikia ni mtunzi bora!, wamekuwa wakihoji toka lini Isha Mashauzi akawa mtunzi wa mashairi ya taarab? leo hii anaonekana akiwa ni miongoni mwa wanaogombea tuzo hiyo!, huku wakiachwa au kutupwa nje kwa watunzi bora kama Haji machano wa zanzibar, Foni chupa, Elhatibu Rajabu na Hemedy Omary!, hiki ni kichekesho tena cha karne!.
Naomba nieleweke kwamba hapa sizungumzii unazi lah hasha! najenga hoja kwa misingi iliyo sahihi kabisa!.Isha mashauzi ni muimbaji na wala bado hajakuwa na uwezo mkubwa wa kushindana na watu katika utunzi. Na kama ameanza kutunga basi imekuwa ni mapema sana kumshindanisha na magwiji wa utunzi hapa Tanzania.
Kipengele cha pili ambacho wadau wana lalama ni juu ya waimbaji wa kiume! mtu kama Mussa kijoti amekiimba nini haswa mpaka awepo katika waimbaji bora wa kiume?, inakuwa unamuacha mtu kama Nassor Hussein "chollo", Hashim Said, Omary tego na wengineo wengi! unakwenda kumuweka Mussa kijoti...hivi ni kweli kabisa!.
Jambo lingine wadau wanaumizwa na ukilitimba wa kamati ya kili music award's kwa kuwapendekeza watu wale wale kila mwaka nikimaanisha wasanii ni hao hao kila kukicha! unataka kutuambia hakuna waimbaji wanaoimba vizuri mpaka kila mwaka kutawaliwa na hao tuu!.
Pia hiyo kamati ya watangazaji ambao ndio imepewa jukumu la kuhakiki majina ya wasanii watakao shiriki mashindano haya yawapasa muongeze idadi yao ili kuleta changamoto zaidi. au ikiwezekana muchukuwe watangazaji toka redio za mikoani pia!.
Naamini sitokuwa adui kwa kusema ukweli kwa yanayotokea!, nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko!.Tukutane tena juma lijalo Ahsante!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni