TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 6 Mei 2015

YOUNG HASSAN ALLY:- WADAU NAOMBA KURA ZENU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Muimbaji nyota anaekuja kwa kasi ya kimbunga Young Hassan Ally wa bendi ya Ogopa kopa classic ametinga ndani ya ofisi za ubuyu wa taarab na kuwaomba wadau wampigie kura katika kinyang'anyiro cha kilimanjaro music award's kinacho endelea kwa sasa.


       Young Hassan Ally anashindania muimbaji bora wa kiume pamoja na mtunzi bora, akizitaja namba zake za kumpigia kura Hassan Ally alisema, wadau wanaweza kunipigia kura kwa namba zifuatazo ili kunipigia kura kuwa muimbaji bora wa kiume...nenda katika uwanja wa sms wa simu yako andika BA4 kwenda 15415, Na kunipigia kura katika utunzi bora pia nenda katika uwanja wa sms wa simu yako alafu andika FA5 kwenda 15415 kwa salio la kawaida na wala sio la kujiunga...kura yako ndio ushindi wangu. Natanguliza shukrani yangu kwenu wapenzi wangu, nawaomba sana zaidi ya sana mniwezeshe niweze kushinda mwaka huu.

YOUNG HASSAN ALLY.

        Uongozi wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unapenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wasomaji wote kumsapoti Young Hassan Ally katika mchakato huu ili aweze kuibuka kidedea kwani huyu ni miongoni mwa vijana wetu wanaokuja vizuri sana katika tasnia hii ya taarab nchini Tanzania kwa sasa!.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni