TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 6 Mei 2015

BLACK KOPA:- SINA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MSICHANA HUYU JAMANI!.


NA KAIS MUSSA KAIS.

               Jina alilopewa na wazazi wake wawili ni Mohamedy Kibwana ila jina la kutafutia ugali katika sanaa anajulikana kama "Black Kopa", huyu ni kijana mtoto wa malkia wa mipasho nchini Tanzania Khadija Omary Kopa.


BLACK KOPA AKIWA NA "ZAYANA" MSICHANA INAESEMEKANA KUWA NI MPENZIWE!.

      Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake mpya uitwao "Fully kuenjoy" ambamo ndani yake kuna msichana mzuri aitwae "Zayana" anaonekana akiwa sambamba kimiondoko na Black kopa jambo lililozua uvumi mkubwa jijini Dar na vitongoji vyake kwamba Black kopa anatoka kimapenzi na msichana huyo, mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com kama kawaida yake ukamuweka kitimoto Black kopa ndani ya sindano tano na mambo yalikuwa kama ifuatavyo:-


UBUYU WA TAARAB:- Mambo vipi Black kopa, nimekuja kwako kuna taarifa nimezisikia zinahitaji ufafanuzi wako, katika video mpya ya fully kuenjoy unaonekana upo na msichana mrembo na taarifa zilizozagaa ni kwamba unatoka nae kimapenzi msichana yule je kuna ukweli wowote hapo?.


BLACK KOPA:- Hapana si kweli sina uhusuano wa kimapenzi na msichana yule, isipokuwa kinachoonekana pale ni sanaa zaidi, unapocheza sehemu kama ile ni lazima uonyeshe uhasilia yaani uwe serious na kazi ili video iwe nzuri, penye kubusu lazima ubusu hata unapotakiwa umkumbatie ni lazima umkumbatie haswa! ili kuleta uhasilia zaidi katika wimbo husika!.


UBUYU WA TAARAB:- Huna muda mrefu sana tokea uingie katika tasnia hii ya uimbaji wa taarab hapa nchini, lakini maendeleo yako yanaonekana kuja kwa kasi zaidi unadhani ni nini siri ya mafanikio yako?.

BLACK KOPA NA ZAYANA!.

BLACK KOPA:- Kwanza nianze kwa kumshukuru mungu kabla sijalijibu swali lako!Lakini siku zote siri ya mafanikio ni kujituma na kuwa mbunifu zaidi, nimekuwa nikijituma sana kwenye kazi zangu, pia namshukuru sana mama yangu kipenzi Khadija kopa kwani amekuwa akinisapoti na kunitia moyo zaidi ili niweze kufikia mafanikio zaidi.


UBUYU WA TAARAB:- Ukiwa msanii wa Ogopa kopa classic unazizungumziaje nafasi ambazo bendi yako imepata katika kinyang'anyiro hiki cha kilimanjaro music award's mwaka huu?.


BLACK KOPA:- Naweza kusema huu ni mwanzo mzuri zaidi kwetu, kwani bendi yetu haina muda mrefu tokea ianzishwe na inaonekana kukubalika zaidi na wapenzi wa taarab nchini na hata nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania, kwa pamoja kama wasanii wa Ogopa kopa tunatoa pongezi kwa wadau na pia nawaomba waendelee kutupigia kura ili tushinde katika vipengele ambavyo tumeteuliwa.

ZAYANA NA BLACK KOPA!!.

UBUYU WA TAARAB:- Hapo nyuma nilikufahamu zaidi katika muziki wa bongofleva wakati ukiwa kule visiwani zanzibar, lakini ulipoibukia huku Bara ukajiingiza katika muziki wa Taarab, unaweza kusema ni kitu gani haswa kilikuvutia kujiunga na tasnia hii?.


BLACK KOPA:- Ni kweli wakati nipo zanzibar nilikuwa naimba bongo fleva zaidi lakini nilikuja kuiacha baada ya kuona kule ni kugumu sana kiukweli, nimesharekodi nyimbo kadhaa katika bongo fleva lakini hazisikiki kuchezwa redioni wala video kuonyeshwa runingani, na alienifanya mimi kuipenda taarab ni marehemu kaka yangu Omary kopa mwenyezimungu amrehemu. Nilikuwa napenda sana uimbaji wake kwakweli.


UBUYU WA TAARAB:- Mwisho una ushauri gani kwa wasanii wenzako, wandishi wa habari na hata viongozi wa taarab kwa ujumla nini cha kufanya ili kuwanyanyua wasanii wachanga kama ninyi na muweze kujulikana kimataifa?


UBUYU WA TAARAB:- Ushauri wangu kwa viongozi wa taarab nchini nawaomba wawe ni watu wa kuwaamini zaidi chipukizi kwani wanakuwa na morali ya kazi zaidi na wanahitaji kufanya mambo makubwa, wandishi sapoti yao kwetu inahitajika zaidi kwani wao ndio wanaotupandisha mpaka watu kutufahamu baada ya kutusoma mitandaoni au hata katika media zingine, wasanii wenzangu nawaomba tupendane na tushirikiane ili tuweze kuufikisha mbali zaidi muziki wetu wa taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni