TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 6 Mei 2015

BAADA YA ZIARA NZITO NA YENYE MAFANIKIO NCHINI "UK" HATIMAE GUSAGUSA WAREJEA NCHINI SALAMA USALIMINI!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Bendi yako ya Gusagusa au wazee wa Dolla, jana majira ya jioni imefanikiwa kurudi nchini Tanzania salama usalimini baada ya kufanya ziara ya nguvu ya wiki moja na yenye mafanikio makubwa nchini uingereza kwa udhamini mkubwa wa Didas fashion kampuni inayomilikiwa na mtanzania mwana dada Khadija aishie nchini humo.


BI MWANAHAWA ALLY NA BI AFUA SULEIMAN WAKIWA AIRPOT.

        Katika mapokezi hayo gusagusa ililakiwa na wandishi wa habari, mashabiki lukuki pamoja na viongozi waandamizi ambao walibaki hapa nchini Tanzania akiwemo Foni chupa katibu wa bendi, mhasibu wa bendi Mr Nassor pamoja na meneja wa bendi hiyo Kais mussa kais.


       Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushuka kwenye ndege mkurugenzi wa bendi hiyo Hassan Farouk aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara yao ilikuwa ni nzuri na yenye mafanikio ukizingatia ni mara ya kwanza bendi yao inafanya maonyesho nchini humo, aliwashukuru wakazi wa UK kwa kujitokeza kwa wingi kwenye matamasha yao lakini vile vile alitoa shukrani kubwa kwa Didas fashion kwa mwaliko huo!.


ABDALLAH NG'ONDA NA BI MWANAHAWA ALLY WAKIWA NDANI YA NDEGE.

      Nae balozi wa kudumu wa Gusagusa min bendi mwana dada maarufu Asya Idarous Khamsin ambae aliambatana na bendi hiyo nchini UK alisema huo ni mwanzo tu kwani bendi ya Gusagusa kwa sasa ni bendi ya kimataifa zaidi, tuna mialiko ya nchi za ujerumani, Marekani, Canada na Oman bila kusahau tupo kwenye mazungumzo na promota mmoja ambae anataka kuipeleka bendi mombasa hivi karibuni alimaliza kwa kusema!.


ASYA IDAROUS, BI AFUA SULEIMAN NA MPIGA KINANDA HAMISI WAKIWA NDANI YA NDEGE.

      Ikumbukwe kwamba Gusagusa ndio bendi ya kwanza nchini Tanzania kuamua kupiga zile nyimbo za zamani ambazo zilianza kusahaulika miongoni mwa bendi zilizopo hapa nchni. kwa sasa Gusagusa min bendi au wazee wa Dolla wana show zao tatu hapa nchini ambazo ni siku ya ijumaa wanakuwa pale Max hall Ilala, siku ya jumamosi huwa wanakuwa pale Lango la jiji magomeni mikumi bila kusahau siku ya jumapili wanamalizia week end yao ndani ya ukumbi wa Hugo house kinondoni karibu na soko la ma-Tx, show zote huwa zinaanza saa tatu usiku mpaka majogoo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni