GUSAGUSA MIN BENDI BAADA YA KUSHUKA AIRPOT YA UK. |
Bendi ya Gusagusa min bendi au wazee wa Dolla ambayo imerejea juzi jioni ikitokea nchini uingereza kwa ziara ya show's mbili matata sana! leo Balozi wa bendi hiyo Mamaa Asya Idarous Khamsin amefika katika ofisi zetu za "SKILLMAN MEDIA" ambayo inaendesha blog hii pamoja na Group's na Page mbalimbali za Taarab hapa nchini ili kutoa shukrani zao za dhati kwa Club Malibu ya London ambayo ilitoa msaada mkubwa wakati bendi ipo kule.
WAKIPATA MSOSI WA NGUVU NDANI YA UK. |
Akizungumza kwa niaba ya bendi nzima ya Gusagusa min bendi Asya Idarous alisema, wakati tupo nchini uingereza Club hii ilitujali na kututhamini sana tu! kuna baadhi ya mambo wametufanyia mazuri tena ya kiungwana zaidi wakishirikiana na Didas Fashion, sisi kama Gusagusa tunasema hatuna cha kuwalipa ila mwenyezimungu tu ndie mlipaji!, milango ipo wazi pia kwa "Club malibu" kama wanaitaka Gusagusa kwenda nchi yoyote ya ulaya kufanya show tupo tayari, kwani waswahili wanasema uungwana ni vitendo alimaliza kwa kusema.
BI AFUA SULEIMAN, BI MWANAHAWA ALLY, ASYA IDAROUS NA MKURUGENZI HASSAN FAROUK NDANI YA UK. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni