NA KAIS MUSSA KAIS.
Asalaam aleykum wasomaji wangu wapendwa, kama ambavyo nimekuwa nikiwajulisha kwamba nitaendelea kufanya maboresho ya habari ambazo zitakuwa zikitolewa na kampuni yangu ya "Skillman media" ambayo inamiliki vyombo vifuatavyo:-
Blog:- ubuyuwataarabutz.blogspot.com
Page:- ubuyu wa taarabu
Page:- Taarabu viwanjani
Group:- ubuyu wa taarab
Account:- pinterest.com.
Na hivi karibuni kuna mambo mazuri zaidi yanakuja tuendelee kuombeana dua inshallah!, Dhumuni kubwa la kuandika habari hii kwenu ni kuwajuza kwamba kuna segment mpya 3 natarajia kuzianzisha hivi karibuni, na kama ilivyokawaida yangu kabla sijaweka hewani ni lazima niwatangazie ili mkae mkifahamu kwani ninyi ni wasomaji wangu wapendwa ambao nawajali na kuwathamini sana!.
Kuna segment 3 ambazo ni "Mjue msanii wako", "Ninavyojisikia" na "Mjue mtangazaji wako"., kila kipengere kina maudhui yake tukianza na mjue msanii wako, hapa tutakuwa tunafanya mahojiano na wasanii mbalimbali toka bendi mbalimbali ili kujua historia zao wapi wametokea ni nani aliemvutia katika taarab na nini malengo yake ya baadae pamoja na maswali kadhaa wa kadhaa!.
Katika kipengele cha ninavyojisikia hapa kwanza napenda niwajulishe kuwa hii segment nimeamua kuiendeleza ili kumuenzi aliekuwa mke wangu marehemu Nyawana kwani kipengere hiki alikuwa nacho katika kipindi chake cha taarab ndani ya "Passion fm" enzi za uhai wake...mwenyezimungu amrehemu Amin!.Hapa mimi kama mwandishi nitakuwa na uhuru wa kuzungumzia chochote kile na sio lazima kiwe kinahusiana na taarab wakati mwingine inaweza kuwa dansi, mchiriku, mduara, vanga, segere, baikoko na aina yoyote ile ya muziki ambao nitajisikia ku-share nanyi wasomaji wangu.
Katika segment ya mjue mtangazaji wako hapa watangazaji watapata nafasi ya kuelezea historia zao wapi wamepitia na nini matarajio yao ya baadae!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni