Bi Eshe Mohamedy muimbaji wa siku nyingi wa taarabu nchini tanzania, usiku wa jana ndani ya ukumbi wa lango la jiji magomeni jijini Dar alishangaza watu kwa sauti yake tamu na maridadi isiyoisha hamu wakati alipokuwa akiimba kwenye onyesho la bendi ya Gusagusa min bendi ambalo hufanyika ndani ya ukumbi huo kila siku ya jumamosi.
BI ESHE MOHAMEDY AKIIMBA JANA KATIKA UKUMBI WA LANGO LA JIJI MAGOMENI. |
Alipanda kuimba wimbo wa kwanza mida ya saa sita na nusu za usiku na kibao kisemacho "Kama ni rahisi" umahiri na ufundi wa kuichezea sauti yake uliwafanya wapenzi lukuki waliojitokeza kwenye onyesho hilo kumuomba tena mkongwe huyo kurudi tena stejini, na safari hii akapanda na wimbo usemao "Haya maumbile yangu"...watu walichanganyikiwa na kuanza kumtunza pesa kama mvua!.
WASANII WA GUSAGUSA MIN BENDI. |
Akizungumzia tukio hilo mdau mkubwa wa Gusagusa min bendi ambae anatambulika kwa jina la Alhabib alisema kwakweli nimeamini vya kale dhahabu! huyu mama ana sauti tamu kiasi hiki! je enzi za usichana wake alikuwaje? mimi amenifurahisha sana kiukweli mungu amuweke, nae mkurugenzi wa bendi hiyo Achun Baa! amesema Bi Eshe Mohamedy atakuwa anapatikana katika shughuli zote za gusagusa min bendi kuanzia sasa na kuendelea, huku taratibu za kiuongozi zikiendelea kufanyika ili kuona tunaweza kufanya nini juu ya mama yetu huyu.
GUSAGUSA MIN BENDI WAKIWA STEJINI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni