TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 17 Mei 2015

KILI MUSIC AWARD'S, KIPENGELE CHA DIRECTOR BORA WA MUZIKI WA TAARAB NCHINI NI MUHIMU SANA!.


  NA KAIS MUSSA KAIS
         0657- 036328.

                 Habari za jumapili wapenzi wasomaji wangu wa blog hii ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com, kama ilivyo kawaida yetu leo tumekutana tena hapa ili tupeane mawili matatu yaliyo ndani ya tasnia yetu hii ya taarab hapa nchini.


     Kumekuwa na mchakato wa kutafuta wasanii bora kwa aina mbalimbali za muziki hapa nchini kupitia kilimanjaro music award's, ila ningependa sana nizungumzie aina ya muziki ambao ndio na-deal nao yaani taarab. kuna hiki kipengele muhimu sana cha muongozaji bora wa muziki wa taarab hapa nchini yaani "Director" kimekuwa kikisahaulika karibia kila mwaka!, labda hii sio kwa makusudi ila academic ya kili music award's hawatambui haswa majukumu ya huyu anaeitwa Director ndani ya muziki huu wa taarab!.


     Katika muziki wetu wa taarab Director ana kazi kubwa sana kuliko hata producer, sisemi haya kwa kuponda u-producer la hasha! ila nataka nifafanue kazi za watu hawa wawili alafu wewe msomaji wangu utajua ni nini namaanisha. Nikianza na Director yeye ndio mtengenezaji wa muziki, sauti, uimbaji na wakati mwingine hadi mashairi, msanii anaweza akaja katika mazoezi akakabidhiwa shairi tu mkononi ambalo limepangwa kwa vina na mizani tu lakini ukimwambia imba unaweza ukacheka!, sasa pale ndipo anapoingia Director na kuanza kutumia akili zaidi kwa kushirikiana na wapiga vyombo kwa kuwaambia piga hivi, wewe imba hivi, ninyi waitikiaji itikieni hivi mpaka wimbo mzima unakuwa umekamilika na kuwa tayari kwa kurekodiwa, hapa zinaweza kupita siku tatu na zaidi wakiendelea kuelekezana kwa pamoja.


    Kwa upande wa pili nikija kwa Producer yeye kazi yake ni kurekodi tu ule wimbo na kuhakikisha unatoka katika ubora ulio mzuri kwa kufanya mixing ya kitaalam zaidi, kazi ya kurekodi wimbo mmoja inaweza kuchukua masaa mawili mpaka matatu na wimbo unakuwa tayari kwa kusikilizwa!.Hapa kuna tofauti ya producer wa muziki wa bongo fleva na producer wa muziki wa taarab, huyu wa bongo fleva ana kazi kubwa sana ya kutengeneza muziki mzima wa muimbaji ambae atakuwa ameenda kurekodi studio, anatakiwa atulize kichwa haswa ili kutoa wimbo ulio bora ili hata ukianza kusikika masikioni mwa watu waseme kweli hapa jamaa amefanya kazi anatengeneza kuanzia beat, vinanda, upigaji wa magita na kadhalika.


    Lakini producer wa taarab yeye hatengenezi chochote zaidi ya maelekezo madogo madogo tu lakini kila kitu kinakuwa kimesha malizwa na Director tokea mazoezini, hapa ndipo linapokuja suala la msingi kwamba hawa ma-director wa muziki wa taarab wanayo haki ya kuwekewa kipengele chao cha Director bora wa mwaka kulingana na kazi kubwa ambayo wanaifanya mpaka kufikia wimbo kukubalika na kupendwa hili sio jambo dogo kisanaa kabisa.


    Academic ya kilimanjaro music award's hebu litazameni hili kwa umakini mkubwa ili muweze kulifanyia kazi kuanzia mwakani, naamini kama tungekuwa na chama cha taarab tanzania kilio hiki kingekuwa kimeshawafikia mapema lakini udhaifu wetu ndio unaotufanya wakati mwingine kukosa haki zetu za msingi kabisa...Daima sitoweza kuwa adui kwa kusema kweli Alamsiki wasomaji wangu wapendwa!.

                        

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni