TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 17 Mei 2015

GUSAGUSA MIN BENDI NDANI YA HUGO HOUSE KINONDONI LEO JUMAPILI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Bendi inayofanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya taarab asilia nchini Tanzania Gusagusa min bendi, leo siku ya jumapili inatarajia kushusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa "Hugo House" kinondoni karibu na soko la ma-tx Dar.


       Show hiyo ambayo imedhaminiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Fabak Fashion bibie Asya Idarous Khamsin ambae pia ni balozi wa kudumu wa gusagusa min bendi itaanza saa mbili kamili usiku hadi majogoo. Akizungumza na mtandao huu Asya alisema leo kutaporomoshwa nyimbo maalum sababu ile ni sehemu ya watu maalum na wastaarabu zaidi

, watu maarufu wamealikwa kuhudhulia onyesho la leo hivyo amewaomba wadau na wapenzi wote kujitokeza kwa wingi sababu kiingilio pia kimepunguzwa kitakuwa ni shilingi 5000/= tu kwa kila mmoja.


   Muimbaji mkongwe Bi Eshe Mohamedy toka visiwani zanzibar akishirikiana na Bi Afua Suleiman nao watakuwepo katika kuwaletea vile vya kale zilivyopendwa zaidi, nyote mnakaribishwa bila kukosa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni