NA KAIS MUSSA KAIS.
Asalaam aleykum ndugu wapenzi na wasomaji wa blog hii bora kwa sasa nchini tanzania, blog pekee inayo zungumzia muziki wetu wa taarab kwa upana mkubwa pasipo kubagua bendi yoyote ile.
Leo siku ya jumamosi tunaianza ile segment yetu ya "Mjue msanii wako" ambayo itakuwa ikikujia siku na wakati kama wa leo, hapa utapata kuwajua wasanii mbalimbali ambao hapo kabla ulikuwa ukiwasikia kijuu juu kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Tunzania.
Aliepata bahati ya kutufungulia segment yetu hii ni Mkurugenzi wa Fungakazi modern taarab ambae anatambulika kama kapten Temba "mwanaharakati asieshindwa kirahisi", kwanza nilitaka kujua kimya chake cha muda mrefu kinaashilia nini? maana wadau wamekuwa wakimuulizia sana!.
KAPTEN TEMBA. |
KAPTEN TEMBA:- Mimi nipo, na bendi yangu ya fungakazi modern taarab ipo, isipokuwa tulikuwa kimya kidogo ili kupanga mikakati ni jinsi gani tunakuja tena kwa ujio ulio bora zaidi ukizingatia tulikuwa kimya kidogo, kuna nyimbo mpya tumeziandaa na baadhi tayari tumeshazifanyia mazoezi bado kuzirekodi tu.
UBUYU WA TAARAB:- Wadau wangependa kujua elimu yako haswa ni ya kiwango gani na je uliwahi kupitia madrasa, maana rafudhi yako inaonekana kama nawe uliwahi kuimba kaswida kaka!.
KAPTEN TEMBA:- Nina elimu ya kawaida tu ya kidato cha nne ambayo niliipata katika sekondari ya kigamboni, vile vile madrasa nimesoma sana, ingawa mimi ni mtoto ambae wazazi wangu wana dini tofauti, mama yangu ni muislam na baba yangu ni mkristo, ila kwa sasa mimi nimeamua kuwa katika dini ya uislam moja kwa moja na hata ndoa yangu na Zainab Machupa imefungwa kiislam.
UBUYU WA TAARAB:- Nilimuuliza katika muziki wa taarab ni nani haswa ambae unaweza kusema kwa namna moja ama ingine alichangia sana kukuvuta wewe kuingia katika utunzi mpaka uimbaji, maana kwa muda mchache sana umekuwa ukitajwa sana midomoni mwa wadau juu ya tungo zako na uimbaji wako mzuri?.
KAPTEN TEMBA NA SENIOR BACHELLAH!. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni