TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 15 Mei 2015

MGENI KISODA:- HUKU NILIPO SASA RAHA, NAJINAFASI WALA SINA WASIWASI!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Wadau, mashabiki na wapenzi wa mwanamuziki Mgeni Kisoda wamekuwa wakipiga simu kwa wingi sana ofisini kwetu wakitaka wafahamishwe kipenzi chao Mgeni Kisoda yupo wapi kwa sasa! maana wamekuwa wakiona kimya kimezidi...hawajui yu wapi kwa kipindi hiki.


MGENI KISODA AKIWA AMESHUKA KWENYE NDEGE TOKEA DUBAI.

     Dawati la habari la mtandao huu lilimtafuta Mgeni Kisoda na kufanya mazungumzo nae ya ana kwa ana!, kwanza tulitaka kujua ni kitu gani haswa kilichomfanya kuwa kimya kwa muda mrefu kitu ambacho sio kawaida yake, alianza kwa kusema Mimi kwa sasa nipo "Yamoto bendi" pamoja na akina Dogo Asley pale napiga kinanda na gitaa la besi kama ujuavyo mimi ni kilaka bab! akacheka kidogo!.

MGENI KISODA AKIWA KWENYE NDEGE NA BEKA WA YAMOTO BENDI.

   Kimya changu ni kwamba tulikuwa kambini tunaandaa nyimbo mpya kali kama ilivyo kawaida ya Yamoto bendi huwa hatubahatishi, baada ya hapo tukasafiri kidogo tukaenda Dubai kwa maonyesho kadhaa kabla ya kuelekea nchini uingereza, ila kwa sasa tumesharejea tupo hapa nchini na tunaendelea na harakati zetu, najua mashabiki wangu wa upande wa taarab watakuwa wamenimiss sana, ila nawaambia wasijali mimi kijana wao nipo na naendeleza michakato yangu kama kawa!, nawakaribisha sana huku yamoto bendi waje tufurahi kwa pamoja.

MGENI KISODA AKIWA MAZOEZINI YAMOTO BENDI.

   Ikumbukwe Mgeni Kisoda alikuwa katika bendi ya Jahazi modern taarab na alikuwa ni mmoja wa wapiga kinanda anae tegemewa sana na mfalme mzee yusuph, lakini baadae alisimamishwa bendi kabla ya kuondolewa kabisa baada ya kusemekana kwamba alionekana twanga pepeta akifanya kazi, huku bendi yake ya Jahazi modern taarab ikiwa kazini, jambo ambalo mwenyewe Mgeni Kisoda alikanusha na kusema ni fitina za watu wachache ambae walikuwa hawataki kumuona akifanya kazi pale Jahazi modern taarab. Kwa sasa yupo Yamoto bendi akifanya yake, huyo ndio Mgeni Kisoda!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni