TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 13 Mei 2015

HASHIM SAID "IGWE":-NAMPENDA SANA FATU CHINA...MAHASIDI NAMKOME!.


NA KAIS MUSSA KAIS.

              Habari zenu wapendwa, kwa wakazi wa Dar na vitongoji vyake napenda niwape pole wale waliofikwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, wasijali naamini serikali yetu inafanya juhudi za kuhakikisha mnapata sehemu nzuri ya kuishi japo kwa muda!.


      Leo tumekutana tena katika Sindano tano za ubuyu wa taarab na tupo na Hashim Saidi "Igwe" muimbaji toka mashauzi classic bendi inayomilikiwa na Isha Ramadhan "Mashauzi", na mazungumzo yetu yalikuwa kama ifuatavyo:-


UBUYU WA TAARAB:- Hashim Saidi mambo vipi, dawati letu la habari limekutembelea ili tuyajue yaliyojificha juu ya kuandamwa kwenu wewe na mkeo Fatu China! kuna tetesi kwamba kuna kundi la watu limeamua kwa makusudi ku-deal na ninyi mpaka wahakikishe mnaachana! sijui taarifa hizi unazo! na unaweza kuwajua watu wenyewe?.

HASHIM SAID "IGWE" MUIMBAJI WA MASHAUZI CLASSIC.

HASHIM SAIDI:- Taarifa hizo nazijua na hata hao watu wenyewe nawajua kwani huwa wanamtumia sana sms za uzushi na uongo mke wangu Fatuma ili aamini wanayo yasema na ikibidi tutengane! lakini nawaambia mke wangu yupo makini na fitina zao zitagonga mwamba...Fatuma mke wangu ananipenda nami pia nampenda.


UBUYU WA TAARAB:- Unaweza kukumbuka kwa mara ya kwanza Fatuma mlikutana wapi na katika mazingira gani?. kwasababu hivi sasa penzi lenu limekuwa ni gumzo midomoni mwa watu mpaka kwenye mitandao!.


HASHIM SAID:- Nakumbuka Fatuma nilianza kumpenda kitambo sana tokea anakuja katika show zetu kama shabiki mpaka nilipo mtamkia kwamba Fatuma nahitaji kuwa wako kimapenzi na ikibidi nikuoe kabisa uwe mke wangu! mwanzoni ilikuwa ngumu kunikubalia, vikwazo vilikuwa vingi sana lakini kilichoandikwa na mungu kimeandikwa tu! baadae tulikuwa pamoja mpaka ndoa ikapita!.


UBUYU WA TAARAB:- Kuna taarifa kwamba hivi sasa unakuja na wimbo mpya kabisa ukiwa na mashauzi classic unaitwa "Tuacheni tulale" eti wimbo huu umeutunga maalum kwa ajili ya mkeo Fatu China ni kweli kiongozi?.


HASHIM SAID  NA MKEWE FATUMA CHINA WAKIWA KATIKA POZI.

HASHIM SAID:- Hizo taarifa ni kweli kabisa kaka, nimeamua kumuimbia mke wangu na kumdhihilishia ni kwa kiasi gani ninavyompenda na kumjali...Nampenda sana Fatu China wangu! yeye ni kila kitu katika maisha yangu kwa sasa, sikumbuki kama nilishawahi kumpenda mwanamke yeyote aliewahi kuwa mpenzi wangu kama ninavyo mpenda Fatuma mke wangu! Namwambia wimbo huu ni maalum kwake na kwa mashabiki zangu wote.


UBUYU WA TAARAB:- Swali la kizushi, unadhani unahitaji watoto wangapi kuzaa na mkeo Fatu China? maana waswahili wanasema maisha ni kupanga na wala sio kukurupuka kama akina mwafulani!.


HASHIM SAID:- Haha haha haaaaaa! mungu atujaalie tupate watoto wawili tu wakike mmoja na wakiume mmoja itakuwa poa sana! wakiume afanane sura na baba yake na wakike afanane sura na mama yake Fatu China mke wa mie!.


UBUYU WA TAARAB:- Mwisho kabisa unawaambia nini mashabiki zako na pia wale wanaoshinda kwa waganga usiku kucha wakitaka kulibomoa penzi lenu wewe na mkeo Fatuma?.


FATUMA CHINA MKE WA HALALI WA HASHIIM SAIDI "IGWE".

HASHIM SAID:- Mashabiki zangu naomba waendelee kunipa sapoti kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila siku, pia wasivunjike moyo kwakuwa mwaka huu sijaingia katika mashindano ya kilimanjaro music award's kwani hata mwakani panapo uhai nitaingia Inshallah, na hawa wanaokesha kulibomoa penzi letu nawaambia wanajisumbua ni bora wafanye mambo mengine kwani penzi letu limeandikwa na mola, mlimwengu katu hathubutu kulitikisa...Nampenda mke wangu Fatuma!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni