NA KAIS MUSSA KAIS.
Leo jumatatu tunaanza kwenda hewani na ile segment yetu mpya ya "Mjue mtangazaji wako" ambayo itakuwa ikikujia kila siku ya jumatatu zote zijazo kupitia hapa hapa katika blog bora ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com.
Na anae tufungulia kipengele hiki ni mtangazaji aitwae Leyla Tot ambae kwa sasa anatangaza pale "TK FM 88.5"mkoani Tanga, kupitia kipindi chake cha taarab kiitwacho Nakshi za pwani kuanzia jumatatu mpaka ijumaa, muda saa kumi kamili mpaka saa moja usiku. Nilianza kwa kumuuliza elimu yake aliipata vipi mpaka kufikia kwenye utangazaji?.
LEYLA TOT AKIWA KAZINI. |
Nae alianza kwa kusema, nimesoma mpaka kidato cha nne nikaenda chuoni pale Dsj nikasomea kozi ya uandishi wa habari na utangazaji pia nimesoma Spliended college and english course. ilipofika mwaka 2005 nilijiunga na kikundi cha maigizo hapo hapo chuoni na tulikuwa na akina Amanda, Pooshy, Mashaka na wengineo wengi nimewasahau ila sikupata bahati ya kurekodi mchezo wowote na kikundi hicho kwani Baba watoto wangu alinikataza kuendelea na sanaa ya maigizo.
Ndipo nikaingia kutafuta kazi na cheti changu, nikafanikiwa kupata kazi C2C TV enzi hizo, nikaanzisha kipindi kinaitwa Ladha za pwani ambacho kilitamba sana enzi zake, pale niliwakuta akina Dk Cheni, Issa Diddy, Wasiwasi Mwabulambo yupo Azam Tv, Emanuel Likuda yupo Clouds redio, Mtitu 5 effect, Baraka kilala na Pendo Ibrahim au Lisa kwakweli tuliishi kama ndugu tulipendana sana.
Mwaka 2008 nikachukuliwa na marehemu Shekhe Yahya Hussein aliekuwa bingwa wa utabibu afrika mashariki na kati tukaanzisha kipindi cha nyota zenu ambacho kilikuwa kinarushwa na Channel ten, pale nilikuwa mimi, Zained na Aisha Mushi, huyu Zained mpaka sasa yupo Channel ten.
ANASEMA HATA U-DJ YUPO FITI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni