TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 23 Desemba 2015

HATIMAE BABU ALLY KICHUPA WA JAHAZI MODERN TAARAB AUAGA UKAPELA NA KUFUNGA NDOA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Mpiga kinanda wa bendi ya jahazi modern taarab babu ally kichupa hatimae ameuaga ukapela siku ya ijumaa iliyopita hapa hapa jijini dar es salaam.

BABU ALLY KICHUPA AKIWA NA MKEWE BI NURU.

            Akizungumza na mtandao huu Babu ally alisema nina furaha kubwa sana kwa kutimiza hili ambalo limetokea kwa amani na upendo mkubwa toka kwa ndugu na jamaa zangu wa karibu wakiwemo wafanyakazi wenzangu.wa jahazi modern taarab unajua mke wangu mimi alikuwa ni mkristo na alikuwa akifahamika kwa jina la happy lakini nimembadili dini na sasa ni muislam anaitwa Nuru mrs babu ally. namshukuru mungu.

BABU ALLY AKIWA KAMKUMBATIA MKEWE.

        Nampenda sana mke wangu na kwa sasa tupo katika fungate inshallah tukimaliza naingia mzigoni kama kawaida, Nae Nuru kwa upande wake alisema kuwa nampenda sana mume wangu na namuomba mwenyezimungu ailinde ndoa yetu ili tuweze kujenga familia kwa pamoja. Mtandao huu unapenda kumpongeza babu ally na bi nuru kwa kupiga hatua kubwa kiasi hicho kwani ni wengi wenye dhamira ya kuoa au kuolewa lakini matokeo yake hupotelea hewani tu!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni