TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 20 Desemba 2015

MSAGASUMU:- NAMSHUKURU SANA MUHESHIMIWA EDWARD LOWASA, AMENIBADILISHA KIMAISHA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Anaitwa msagasumu waukweli, kabali yao, mfalme wa uswahilini na majina mengine mengi ambayo nikianza kuyaorodhesha nitamaliza siku nzima.


        Huyu ndio ameufanya muziki wa uswahilini kupewa hadhi na kuanza kuchezwa katika redio stesheni mbalimbali hapa bongo, ukipata bahati ya kukutana nae mwenyewe utapenda kwani ni mcheshi sana asiejua kukasirika, yeye ni mtu anaeheshimu kazi kuliko majigambo na majisifu, anaanza kwa kusema kuwa hapo awali hakutegemea kabisa kama siku moja atakuwa muimbaji na atendesha maisha kupitia muziki.

MSAGASUMU-MFALME WA USWAHILINI.


          Mungu wa ajabu sana na namshukuru sana zaidi ya sana kwa hiki anachonionyesha, mimi nilikuwa ni mtoto wa uswahilini nisie na mbele wala nyuma ila shughuli za kupigisha disco katika sherehe mbalimbali za harusi ndio sababu ya mimi kuianza safari yangu ya muziki mpaka hapa nilipo, baada ya kurekodi nyimbo kadhaa kwa beat za nyimbo za watu za taarab, watu wakaanza kunielewa nini nafanya nini ndipo walipojitokeza watu kadhaa wakanishauri ni vyema nikatengeneza beat yangu mwenyewe nikaimba sababu uwezo ninao, nashukuru niliufuata ushauri wao na mpaka sasa situmii beat za watu tena kama awali narekodi mwenyewe.


         Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu 2015 mimi ni miongoni mwa wasanii tuliokuwa ukawa tukimsapoti muheshimiwa edward lowasa, kwa kuzunguka nae sehemu tofauti tofauti za nchi hii nimeweza kupata usafiri wangu mwenyewe si haba na mambo mengine ya kimaendeleo ambayo nisingependa kuyaweka bayana, napenda kuchukuwa nafasi hii kumshukuru sana muheshimiwa na mungu ampe uhai mrefu zaidi alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni