TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 20 Desemba 2015

RATIBA YA SHOW ZA MAJA'S MODERN TAARAB KATIKA KUSHEREHEKEA X-MASS NA MWAKA MPYA HII HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Bendi yako ya maja's modern taarab leo kupitia mkurugenzi wake hamisi majaliwa imeanika wazi ratiba ya show zao katika kusherehekea sikukuu za x-mass na mwaka mpya.


HAMUYAWEZI KONDO-MUIMBAJI WA MAJA'S MODERN TAARAB.

            Akizungumza na mtandao huu, majaliwa alisema kwamba bendi yake kwa sasa ipo kamili gado na inaanza rasmi maonyesho yake kuanzia x-mass hii na burudani hii itaendelea katika kumbi zingine. siku ya tarehe 25/12/2015 siku yenyewe ya sikukuu bendi hii itakuwa maeneo ya mbezi beach kwa shughuli maalum ya
mahafari ya moja ya chuo maarufu ambapo wanachuo baada ya kupokea vyeti vyao ndipo watapata burudani toka maja's modern taarab mpaka majogoo.


           Siku ya tarehe 26/12/2015 yaani "boxing day" bendi hii itakuwa katika ukumbi wa Jm hotel uliopo pale manzese jijini dar, na siku ya tarehe 27/12/2015 bendi hii itakuwa katika ukumbi wa basihaya huko boko nje kidogo ya jiji la dar, wadau na wapenzi mnaombwa kujitokeza kwa wingi sana kupata burudani ya nguvu toka kwa vijana hawa, ikumbukwe kuwa maja's modern taarab siku za hivi karibuni imeweza kuwachukuwa waimbaji wawili wa bendi ya wakaliwao ambao ni hamuyawezi kondo na farida kindamba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni