TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 20 Desemba 2015

X-MASS DAY- NANI ZAIDI KATI YA COAST MODERN TAARAB NA DAR MODERN NDANI YA MASAI PARK KIBAHA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Katika kile kinachoonekana kupania kufunikana bendi mbili zenye ubora dar modern na coast modern taarab zitafanya onyesho la pamoja siku ya sikukuu ya x-mass ndani ya ukumbi wa masai park uliopo maeneo ya kibaha.


DAR MODERN TAARAB.

          Akizungumza na mtandao huu mratibu wa onyesho hilo mlamali adam alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya nguvu sana kwani karibia bendi zote zimepania kufanya vizuri, vile vile kutakuwa na vijana wa baikoko toka tanga ambao watawaburudisha wakazi wa kibaha na vitongoji vyake, wapenzi wameombwa kufika kwa wingi na wala wasihofie kukatika kwa umeme kwani jenereta kubwa lipo na litafanya kazi kama umeme utakatika.


COAST MODERN TAARAB.

           Nae omary tego mkurugenzi wa bendi ya coast modern taarabalisema kwamba sambamba na wao coast na dar modern lakini pia vijana wa vijukuu wa tego nao watakuwepo pia, ikumbukwe siku hiyo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu saba tu "7000" kwa tiketi moja wote mnaombwa kufika kwa wingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni