TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 13 Machi 2016

HASSAN FAROUK:- KUACHWA KATIKA SAFARI YA NCHINI COMORO NDIO SABABU YA HAMISI CHIZI KUACHA BENDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Siku chache baada ya mtandao huu kuandika habari za Hamisi chizi mpiga kinanda wa zamani wa bendi ya gusagusa min bendi kuondoka, leo mkurugenzi wake Hassan farouk amefunguka mbele ya dawati la mtandao huu. 


HASSAN FAROUK MKURUGENZI WA GUSAGUSA MIN BENDI.

         Akizungumza kwa kujiamini zaidi hassan farouk alisema kuwa ameshangazwa sana na maneno aliyoyazungumza Hamisi kuwa bendi ilikuwa haimjali wala haimthamini kitu ambacho sio kweli kabisa, sababu kubwa ndugu mwandishi ni kuachwa kwa Hamisi chizi katika safari ya nchini comoro ambapo tuliondoka na Hassan soud nae hamisi chizi kubakia hapa tanzania. anashindwa kukumbuka kuwa ile safari ya uingereza ambayo gusagusa tulisafiri tulienda nae yeye na mwenzake hassan soud akabakia tanzania.

 

         Yule ana roho mbaya hataki mwenzie apate!, mimi kama mkurugenzi wa gusagusa nasema kuwa hamisi tulikuwa tunamlipia nyumba milioni mbili kwa mwaka, maji bure, umeme bure!, lakini nilipokuwa namuona anafanya kazi na bendi zingine ikabidi tusitishe huduma ya kumlipia umeme tukamwambia awe analipa mwenyewe umeme! sasa hapo kama anasema ilikuwa inafikia wakati analala kiza ni juu yake mwenyewe maana sisi kama uongozi tulishamueleza,

 

     Jambo lingine amesema kuwa alikuwa anatukanwa matusi tena mbele za watu, labda niseme kuwa hakuna asienijua mimi Achun kwa masihara, na hamisi hataki kuambiwa jambo kabisa anataka kile anachokitaka yeye basi akifanye anashindwa kuelewa kuwa yeye ni msanii tu na sisi ni viongozi wake, ubaguzi alionao kama pia ataupeleka huko aljazeera alipokwenda basi namtabilia hatokaa atatafuta kwa kwenda!.

 

  mimi naweza kusema kuwa nimemsaidia sana Hamisi katika kipindi alichokuwepo hapa gusagusa lakini hakumbuki fadhira!, namtakia mafanikio huko alipoenda ila akumbuke kuwa hii ni gusagusa bhana huwa hatuteteleki hata kidogo, ameondoka yeye, lakini mpaka sasa tuna wapiga vinanda watatu na kazi inaendelea kama kawaida, hivyo wadau na mashabiki zetu msiwe na wasiwasi bendi ipo makini na show zinaendelea kama kawaida. Kwahiyo naweza kusema kikubwa kilichomuondoa hamisi chizi hapa ni kukosa safari ya nchini comoro na wala sio kitu kingine asiwaongopee watu alimalizia kwa kusema mkurugenzi huyo!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni