TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 15 Machi 2016

KWA STYLE HII JAHAZI MODERN TAARAB ITAENDELEA KUFANYA VIZURI KILI MUSIC AWARD'S DAIMA MILELE!.

NA KAIS MUSSA KAIS
.


      Asalaam aleykum wasomaji wa ubuyu wa taarab africa na duniani kwa ujumla, leo twende sambamba katika makala hii ambayo italenga zaidi ufanisi wa kazi kwa viongozi wa bendi za taarab nchini.


        Kumekuwa na malalamiko kila inapofikia muda wa lile tukio kubwa la kutafuta bendi bora nyimbo bora na kadhalika "kilimanjaro music award's hususani katika tasnia ya taarab hapa nchini tanzania, bendi nyingi zimekuwa zikilalamika kuwa bendi ya jahazi modern taarab imekuwa ikipendelewa na waandaaji. Mimi nasema si kweli, jahazi wanajitambua sana, nasema hivyo kwanini?, twende sawa hapa naamini nitaeleweka tu!.


      Kilimanjaro music award's huwa mchakato wake mara nyingi mwezi wa nne au zaidi kidoogo kulingana na kalenda ya waandaaji husika, na kikubwa kinachoangaliwa ni nyimbo ambazo zimeweza kutamba mwaka mmoja uliopita kupitia media mbalimbali hapa nchini, wanachofanikiwa viongozi wa jahazi modern taarab ni kusoma alama za nyakati tu kulingana na muda wa shindano jambo ambalo viongozi wa bendi zingine wamekosa kung'amua hilo, ukifanya uchunguzi muda ambao jahazi modern taarab wanaachia nyimbo zao mpya utakuta zina muda zaidi ya miezi sita mpaka nane wa kuchezwa nyimbo hizo katika media mbalimbali, sasa inapofikia kilimanjaro music award's inakuta nyimbo za jahazi modern taarab ambazo zinaendelea kufanya vizuri ni zaidi ya tatu au nne redioni na kwenye televisheni mbalimbali.


      Kwa upande wa viongozi wa bendi zingine hata kama wataweza kurekodi albam nzima yenye nyimbo 5 au 6 basi wimbo utakaopelekwa redioni ni mmoja au miwili, huku zingine zikiendelea kusubiri foleni, sasa kwa style hii ndipo wanapofeli! maana huwezi kujua kila mtu na bahati yake labda hiyo nyimbo ambayo viongozi wameamua iendelee kusubiri ndio ingeshika na kuweza kufanya vizuri mpaka kushinda tuzo!, Mzee yusuph pamoja na viongozi wake wameiachia albam ya kaning'ang'ania ng'ang'ani muda mrefu sana, tena nyimbo zote katika albam zinapigwa maredioni, huu ni ujanja na ni akili ya kazi. nawapongeza sana kwahilo!.


      Acheni uoga viongozi!, na pia kuna tabia ya kumuangalia mzee yusuph kafanya nini na kukaa mna mjadili huku yenu yakiwapita, kwanini msikae na kubuni nyimbo nzuri ambazo zitatangaza bendi yenu?, mimi nazungumza haya sababu nami ni kiongozi wa bendi, hebu tubadilike, mzee yusuph ana viongozi bora na washauri wazuri ambao wanajielewa na pia nyimbo za jahazi modern taarab zimekuwa zikifanya vizuri katika redio mbalimbali sababu ni nzuri, hapa kuna bendi kama ogopa kopa, mashauzi classic na wakaliwao modern taradance, hizi ndizo bendi ambazo kidogo zinaweza kufanya vizuri ingawa bado nako kuna ule udhaifu wa kumfuatilia mzee yusuph huku tukiacha kufanya yetu na hii ni kasumba ya viongozi wengi wa taarab nchini, yaani kukaa mbele ya hadhara na kukili kuwa jahazi modern taarab walipaswa kushinda ni ngumu sana kwetu...kwanini lakini tumekuwa hatuna mapenzi na wale waliofanikiwa?


         Kilimanjaro music award's inakuja tena mwaka huu, wadau na mashabiki tusubiri kuona jahazi modern taarab ikiendelea kufanya vizuri nasi viongozi kuendelea kununa na kutokubali kinachotokea mbele yetu, huu ni mtazamo wangu na hii ndio hali halisi...TUNGOJEE TUONE!!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni