TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 15 Machi 2016

UONGOZI WA ALJAZEERA MODERN TAARAB WATOA TAMKO LAO KUHUSU TUHUMA ZA USHIRIKINA ZINAZOZUNGUMZWA MITANDAONI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Uongozi wa bendi ya aljazeera modern taarab yenye maskani yake kariakoo jijini dar es salaam, leo wametoa tamko lao rasmi kulingana na maneno yanayo endelea kuzungumzwa juu ya ushirikina katika mitandao ya kijamii juu ya bendi hiyo na kiongozi mmoja wa gusagusa min bendi.

        Wakizungumza na mtandao huu walisema kuwa sisi hatuna haja ya kulumbana na mtu yeyote, kwanza sisi muziki hatufanyi kama kazi ila ni burudani tu, tumeanza kusaidia mabendi mbalimbali kipindi kirefu sana mfano babloom, bembea na hata all star's na tulikuwa tunatoa pesa zetu mfukoni na hazirudi kwa style yoyote ile, sasa tuanze kwenda hapo lango la jiji na kufukia sijui uchawi sijui mambo gani! kwa kutaka nini haswa? hatuna shida na wala hatufikilii kuyafanya hayo kabisa!.

      Unajua ndugu mwandishi ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa kwa sasa inaonekana wazi upinzani upo haswa kwa bendi hii yetu ya aljazeera modern taarab na hao gusagusa na imezidi haswa baada ya sisi kumchukuwa mpigaji wao kinanda Hamisi chizi. Sisi aljazeera tunapenda kuwaambia hao viongozi wa bendi ya gusagusa kuwa hatufikirii kufanya lolote juu yao, maana sisi tuna kazi zetu na wala hatutegemei muziki na wala mapato ya mlangoni au kugombania tunza!,. sisi tungefurahi kama na wao wangerekodi nyimbo mpya kama ambavyo sisi tumefanya, huo ndio ushindani wa maendeleo, wasiogope kutuiga, watuige tu! maana sisi tumeanza na wao wafuate!.

      Tupo katika hatua za mwisho mwisho kurekodi nyimbo zetu mbili zingine baada ya kurekodi zile za kwanza mbili, pia wiki ijayo tutaanza kufanya shooting ya hizi nyimbo zetu mpya ili wadau watambue ujio wetu huu mpya sio wa zima moto!. Tuna mipango endelevu sio mchezo! sisi tutawajibu kwa kazi zetu nzuri tu na wataelewa, wajiandae haswa kushindana na aljazeera modern taarab wasitegemee mtelemko kama zamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni