TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 15 Machi 2016

USIKU WA JAMVI LA JIJI NA DAR MODERN TAARAB KILA IJUMAA NDIO HABARI YA MJINI KWA SASA!.

Na pambe za taarab.

            Bendi yako ya dar es salaam modern taarab yenye maskani yake magomeni mikumi jijini, kwa sasa imeliteka jiji kwa show yake bab-kubwa! walioipa jina na "usiku wa jamvi la jiji" ambayo huwa inafanyika katika ukumbi wao wa dar modern hall kila siku ya ijumaa.

       Akizungumza na mtandao huu msanii tegemeo wa bendi hiyo Hassan vocha alisema kuwa show hii ni tofauti na show zingine zote ambazo bendi zingine wanafanya, kwanza ukianzia kwenye mandhari yenyewe ndani ni kusafi sana kunanukia manukato, full A/C, huwa kunatandikwa majamvi mapya kabisa, na hata viti vilivyo pambwa vyema pia huwa vinakuwepo, kwahiyo wale wanaopenda kukaa chini huwa wanakaa na wale ambao wanapenda kukaa katika viti pia wanakaa, kwa upande wa toilet ni kusafi kupita maelezo, kila mtu anapotoka chooni basi kuna mtu maalum ambae huwa anakwenda kusafisha na kumwagia manukato.

MASHABIKI WAKISEREBUKA KATIKA USIKU WA JAMVI LA JIJI IJUMAA ILIYOPITA.

    Hii haijawahi kufanywa na bendi yoyote hapa mjini hususani hizi zinazopiga old is gold, njoo ujionee ijumaa hii na kamwe hutojutia kiingilio chako, tumejipanga kuleta mageuzi katika muziki wetu wa taarab na kwa upande wetu sisi dar modern taarab tunaweza, kwa upande wa burudani huwa tunachanganya radha, pamoja na kupiga nyimbo zetu wenyewe lakini pia huwa tunapiga nyimbo za zamani na mpenzi unaruhusiwa kuchagua ukapigiwa sababu wewe mteja kwetu una thamani kubwa sana alimaliza kwa kusema.

     Wandishi wa mtandao huu ijumaa ya wiki hii wamepata mwaliko rasmi wa kwenda kuhudhulia onyesho hilo maalum la "usiku wa jamvi la jiji" na kile ambacho kitajili basi tutawaletea hapa hapa wasomaji wetu wapendwa!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni