TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 29 Machi 2016

MZEE YUSUPH AKANA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA U-FREEMASON, ATHIBITISHA FATUMA ALLY MAMA SHUGHULI AMEIHAMA BENDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

MKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB MFALME MZEE YUSUPH.

        Asalaam aleykum wapendwa wasomaji wangu, leo nawaletea tena mfululizo wa kile kinachotokea kule katika group la whatsap liitwalo "ubuyu wa taarab" ambalo ni maalum kwa watangazaji wa taarab tu afrika mashariki.

 

      Siku ya jana katika kile kipengele cha "kikaangoni wiki hii" tulikuwa nae mkurugenzi wa jahazi modern taarab mfalme mzee yusuph, ijapokuwa tulichelewa kuwa nae kundini kutokana na sababu zilizo nje na uwezo wetu lakini ilipofika mida ya saa mbili usiku tuliunga nae na maswali toka kwa watangazaji yakawa kama ifuatavyo:-

 

    SALEH TI FM DAR:- Kuna habari kuwa fatuma ally au mama shughuli amehama bendi na moja ya sababu zilizopelekea yeye kuhama bendi ni kuwa ameondoka na pesa za mchezo milioni mbili zikiwemo laki sita zako je ni kweli?.

 

   MZEE YUSUPH:- Swali lako nalijibu kama ifuatavyo, ni kweli fatma amehama bendi lakini amehama kwakuwa hayupo dar es salaam, lakini hizo laki sita sijui laki ngapi ni maneno ya wanafiki tu, kwanza yeye hakuwa kijumbe, mimi laki sita nitamdai ya nini? namudumia pesa nyingi sana zaidi ya hizo laki sita na hawezi kuhama kwa vipesa vidogo hivyo kwahiyo hiyo taarifa sikweli.

 

BLANDINA TK FM TANGA:- Mimi ningependa kujua toka kwa mfalme mzee yusuph ni kwanini siku hizi nyimbo za bendi yako umeamua kuzipunguza dakika?

 

  MZEE YUSUPH:- Kupiga nyimbo ikiwa fupi ikiwa ndefu, inategemea na nyimbo yenyewe malengo yake, na tunafanya hivyo ili nyimbo zetu zipigwe kila pahali ndio maana baadhi zimepunguzwa dakika lakini kwa sasa wimbo wenye dakika tano ni mmoja tu kaning'ang'ania peke yake.

 

 MALICK HITS FM ZNZ:- Mzee yusuph kuna taarifa kwamba ndani ya bendi yako wasanii wanarogana sana na hapo kwenye bendi yako panaonekana ni chuo cha marogaji!.

 

MZEE YUSUPH:- Alijibu kwa ufupi tu...inasemekana pia watangazaji mnarogana sana, sasa ikiwa huku jahazi modern taarab ndio chuo basi naona huko kwenu ni madrasa pia!.

 

EDNA AFM REDIO DODOMA:- Mfalme ni lipi kubwa lililokufanya upige marufuku nyimbo zako kupigwa na baadhi ya bendi au mtu kuimba huoni kama unawaumiza wale wanaotamani kuwa kama wewe?.

 

 MZEE YUSUPH:- Hii ni sheria na imetangazwa na serikali wala sio mimi! hizi ni sheria za hati miliki Edna, mimi naumiza kichwa kutengeneza nyimbo alafu wewe unakuja kupiga copy kirahisi krahisi tu haiwezekani! mimi siruhusu kwa nyimbo zangu.

 

 MWAJUMA RAS FM DODOMA:- Kwanini wasanii wa jahazi modern taarab wanakuwa na malingo sana haswa wanapokuja huku mikoani ukiwaomba waje studio kwa ajili ya interview basi atakuja mmoja au wawili hivi hamuoni kuwa mnapoteza mashabiki wenu?.

 

 MZEE YUSUPH:- Kichuna mtoto ya moro ni kwamba mara nyingi tunaposafiri mfano tunakuja hapo dodoma tunasafiri usiku kwahiyo tukifika wasanii wanakuwa wamechoka wanafikia kupumzika kwa ajili ya maandalizi ya show baadae, ila usijali tunaanda "interview tour special" kwa ajili ya redio na televisheni zote nchini hii itaondoa kiu kwenu watangazaji kwani mtapata muda mrefu wa kuwahoji wasanii wa jahazi kwa kipindi kirefu sana.

 

 KAKA ZEMA CITIZEN REDIO NAIROBI:- Swali langu ni kuhusiana na kuhusishwa kwako na freemason ama liluminati...je ushawahi kuwa mwanachama ama uko na nia ya kuwa mwanachama wa madhehebu hayo?.

 

 MZEE YUSUPH:- Mimi sijui kama kweli hiyo freemason ipo kweli, na kama ipo kweli mbona hawaniuwi nami nimesema waniuwe? na ndio nasema kuwa hakuna freemason, hii ni imani yako tu ukipenda ushirikina basi ndio imani yako na ufreemason wako, kama kweli mimi ni freemason mbona naenda kupiga show mikoani napanda gari kawaida kama wengine? kwanini nisipande ndege? na wanasema freemason wana pesa? hakuna kitu kama hicho kaka zema.

 

 WARDA CHANDE PASSION FM DAR:- Mzee unapopeleka kazi zako redioni basi jitahidi usibague redio peleka kote nasio kama ufanyavyo sasa kuna baadhi ya redio ndio unaona bora zaidi kuliko akina sie!.

 

 MZEE YUSUPH:- Mimi nimemuweka mtu maalum aitwae Haji mabovu huyo ni meneja msaidizi na ndio ambae anasambaza nyimbo zote za jahazi modern taarab, kwahiyo huyu akikuletea nyimbo juwa uongozi wa jahazi modern taarab umeleta nyimbo hapo passion fm mimi siwezi kufanya hivyo kubagua redio na kuzipendelea zingine hapana nawapenda wote!.

 

MARIA KWIZERA FM NGARA:- Swali langu ni kwanini albam yako ya chozi la mama haikufanya vizuri tofauti na zilizopita?, pia ni kwanini wasanii wa muziki wa taarab hawana uongozi ambao unawajumuisha kwa pamoja tofauti na wasanii wa nyimbo nyingine?.

 

 MZEE YUSUPH:- Albam ya chozi la mama haijafanya vizuri una uhakika?, ndio albam iliyochukuwa albam bora ya mwaka, humo kuna nyimbo ya amigo tiba mapenzi, hasidi hana sababu, aso kasolo ni mungu zote zimefanya vizuri sana zaidi ya sana, kuhusu uongozi mimi sielewi, bendi yangu ina uongozi labda kama umemaanisha chama cha taarab kitu ambacho hakiwezekani maana muziki wa taarab walio wengi ni wanafiki tu kamwe hatuwezi kukaa pamoja!.

 

     Maswali yalikuwa mengi sana toka kwa watangazaji wa taarab na tulienjoy sana kiukweli kwakuwa na mfalme mzee yusuph, labda nitoe hitimisho tu la kile kilichofanyika jana kwanza hongera sana mfalme kwa ushirikiano wako kwa watangazaji hukuwa na malingo na ulijibu maswali yote kwa ufasaha kabisa, vile vile nawapongeza watangazaji wote mliopata nafasi ya kushiriki kuuliza maswali kwa mzee yusuph tukutane tena jumatatu ijayo je unajua tutakuwa na msanii gani? tuendelee kuwa pamoja!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni