TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 27 Machi 2016

MUSTAPHA RAMADHAN AFIWA NA MKE WAKE KIPENZI, MAZISHI KUFANYIKA LEO SAA SABA VISIWANI UNGUJA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


        Mkurugenzi wa bendi ya MR modern taarab yenye maskani yake mabibo jijini dar Mustapha ramadhan amepatwa na msiba mzito wa kuondokewa na mke wake kipenzi mwajuma fumo muda mchache uliopita huko zanzibar.


    Dawati la habari la mtandao huu bora kabisa hapa tanzania kwa habari za taarab ulipata habari hizi na mara moja tulimtafuta mwenyewe mustapha ramadhan ili kuthibitisha taarifa hii nae alikuwa na haya ya kusema:- Ni kweli mke wangu mwajuma fumo amefariki muda mchache uliopita na mwili wa marehemu upo visiwani unguja maeneo ya magomeni alipokuwa akiugua.


      Marehemu mke wangu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya kizazi kwa muda mrefu kidogo na tulijitahidi kuhangaika huku na huku juu ya matibabu yake lakini siku zote wanasema kazi ya mungu haina makosa, mimi kwa sasa nipo dar ila najiandaa kuelekea unguja kumsitiri mwenzangu katika safari yake ya mwisho na mazishi yatafanyika leo saa saba mchana maeneo ya huko huko magomeni visiwani unguja, kiukweli inaniuma sana sababu marehemu alikuwa ni zaidi ya mke kwangu, na mpaka umauti unamfika tulikuwa tumejaaliwa kupata watoto wanne, namuombea kwa mwenyezimungu ampumzishe kwa amani marehemu mke wangu kwani nilikuwa nampenda sana alimalizia kusema kwa uchungu mkubwa.


      Mustapha ramadhan ni msanii mkongwe katika tasnia hii ya taarab hapa nchini kwani kabla ya kufungua bendi yake ya MR modern taarab alikuwa ni muimbaji na mtunzi mzuri katika bendi ya muungano culture troup enzi hizo, na kwa kukukumbusha tu mustapha ramadhan ndie ambae aliimba nyimbo za "ubaya hauna kwao na wimbo mwingine ni mambo bado". uongozi mzima wa mtandao huu tunapenda kumpa pole mustapha ramadhan kwa msiba huo mzito uliomfika na mwenyezimungu amfanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni