TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 20 Machi 2016

WATANGAZAJI WA TAARAB KWA PAMOJA KUMUWEKA "KIKAANGONI" KHADIJA OMARY KOPA LEO KUANZIA SAA MOJA USIKU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa leo anatarajia kuingia mikononi mwa watangazaji wapatao 90 wa taarab nchini katika kile kipengele cha "kikaangoni wiki hii" ndani ya group la whatsap ambalo humo ni maalum kwa watangazaji wa taarab tu kutoka afrika mashariki na kati.


MALKIA WA MIPASHO KHADIJA OMARY KOPA.

      Group hilo chini yake admin mkuu kais mussa kais limejiwekea sagment mbalimbali ikiwemo mada mbalimbali za kila siku, vile vile ipo hiyo ya kikaangoni wiki hii ambayo kila ifikapo jumatatu saa moja kamili usiku msanii huingizwa katika group hilo na kujitambulisha na pia kutoa salamu kwa watangazaji hao, ndipo utaratibu wa kuuliza maswali unapoanza!, msanii mwalikwa kwa siku hiyo kama itakavyokuwa kwa khadija omary kopa leo anatakiwa kujibu maswali ya watangazaji hao kwa "voice note" ili waweze kufanyia vipindi vyao baadae unapoisha utaratibu wa maswali.


KHADIJA OMARY KOPA.

       Leo itakuwa patashika nguo kuchanika kwani watangazaji waliopo katika group hilo wana hamu kubwa ya kumswalika malkia wa mipasho nchini tanzania, maana hapa kati kuna mengi sana yamepita na yamesemwa pia, kwahiyo hii ni nafasi pekee kwa wao kupata majibu hayo yote yanayozungumzwa tena live!, kama ilivyo ada yatakayojadiliwa huko ikiwemo maswali na majibu basi dawati la habari la mtandao huu litawaletea hapa kama ilivyo taratibu.Watangazaji ambao bado hawajiunga na group hili na mnapenda kupata material yaliopo humu kundini basi mnaweza kutuma namba zenu kupitia namba hii 0657-036328 ili muunganishwe!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni