TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 20 Machi 2016

DUA YA KUWAOMBEA WASANII WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA FIVE STARS KUFANYIKA LEO MSIKITI WA MTORO KARIAKOO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Kama ilivyo ada kila mwaka kufanya kisomo maalum cha kuwaombea heri wale marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya five stars, basi leo jumatatu tarehe 21/3/2016 pale katika msikiti wa mtoro kariakoo baada ya sala ya saa kumi alasiri kutakuwa na kisomo kwa ajili yao.

       Akizungumza na mtandao huu muandaji wa shughuli hiyo Ally J ambae alinusulika katika ajali hiyo alisema kuwa maandalizi yote yameshakamilika kinachotakiwa ni kwa watu kujitokeza kwa wingi msikitini hapo kuanzia saa kumi ili baada ya kusali tutaanza kwa pamoja kuwaombea marehemu wetu ambao walikuwepo katika ajali hiyo na hata wale ambao hawakuwepo katika ajali hiyo kikubwa ni kuweka nia tu!

   Huu sasa ni mwaka wa tano tokea kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya wasanii 13 na wengine kujeruhiwa, mtandao huu unaungana na wale wote walioguswa na tukio lile na kuwapa pole na pia dawati la habari la mtandao huu litakuwepo msikitini hapo katika kushiriki kwa pamoja dua hiyo!.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni