TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 16 Machi 2016

YOUNG HASSAN ALLY:- AMINA MNYALU ALIKUWA MPENZI WANGU SANA TU!, LAKINI......................

NA KAIS MUSSA KAIS.


YOUNG HASSAN ALLY AKIWAPAGAWISHA WAPENZI WAKE.

        Muimbaji wa bendi ya ogopa kopa classic young hassan ally siku ya jumanne aliwekwa kikaangoni katika group la watangazaji wa taarab la whatsap liitwalo "ubuyu wa taarab" na kuulizwa maswali kadhaa wa kadhaa toka kwa watangazaji tofauti.


   Hassan ally alionekana kujibu kwa kujiamini sana jambo lililowafanya watangazaji hao kulidhika na kumsifia kwa majibu yake, mtangazaji wa kwanza kuuliza swali siku hiyo ni.

 

  MWANAISHA REDIO 5 ARUSHA:- Umekuwa mtunzi wa taarab kitambo sana, je ni nini kinakusababisha hupandi chati kama watunzi wengine, na je wewe kama mtunzi inakuwaje hatujawahi kusikia taarab au wimbo unaozungumzia wanaume kuchukuliana wanawake ina maana hili halionekani?

 

 HASSAN ALLY:- Dada mwanaisha kuhusu mimi kutokupanda chati katika utunzi nasema hayo ni mambo ya mwenyezimungu, yaani mungu akitakata upande zaidi ya waliopanda basi inwezekana, lakini tukija kwenye upande wa utunzi nitaufanyia kazi utunzi wa aina hiyo ili tu kuupeleka mbele muziki wetu wa taarab nchini.

 

TINNA WA EBONY FM IRINGA:- Hassan ally, swali langu kwako nimewahi kusikia unatoka kimapenzi na muimbaji mwenzio aitwae Amina mnyalu je ni kweli ndio wifi yetu?, pili inasemekana Hassan ally unashiriki kale kamchezo kajinsia moja je kuna ukweli wowote hapo?.

 

  HASSAN ALLY:- Alicheka kisha akajibu kuwa Amina mnyalu alikuwa ni mpenzi wangu lakini kwa sasa ni dada yangu mapenzi yaliishaga zamani, kuhusu swali lako la pili ni kwamba sijawahi kufanya huo mchezo ni maneno ya watu tu hayo!.


REHEMA NYAMAKA REDIO ONE:- Unafikiri ni kwanini watu wakuhisie kuwa na mchezo huo Hassan?, na pengine ukisikia kashfa kama hiyo ya ukaka poa unachukuliaje?.


 HASSAN ALLY:- Dada rehema nyamaka naomba nikujibu kama ifuatavyo, nafikiri sio peke yangu ambae nahisiwa hivyo lakini kwa mimi sijali kama watu wakihisi kitu kwangu ikiwa sifanyi.


ASHA VICTORIA FM MUSOMA:- Swali langu kwako ni hili, bendi zimekuwa nyingi hivi sasa, unajipangaje kuwa moja ya bendi bora mbele ya bendi hizo? na vipi kuhusu wasanii wakubwa katika bendi yako?.


 HASSAN ALLY:- Swali lako nalijibu hivi bendi kweli zipo nyingi na mimi ni mtunzi ambae nafahamika, naweza kutengeneza muziki, naweza kutengeneza sauti naweza ku-direct wimbo mpaka unakamilika kwahiyo kwa kazi hii ninajiamini na nitakuja kupigana vizuri, na kuhusu waimbaji wakubwa hakuna muimbaji amefikia ukubwa bila kuanza chini kwahiyo mimi nitawachukuwa wasanii wadogo na nitapanda nao kwa uwezo wa mungu.


 SALMA MAISHA FM DODOMA:- Hivi hassan ally umeoa? na kama bado una mpango gani maana umri unakwenda ndugu yangu!.


 HASSAN ALLY:-  Kuhusu masuala ya kuoa ni kwamba, napanga kufanya hivyo lakini ni vyema nikapata mwanamke mzuri ambae atanifaa, na kuoa ni mpango wa mungu, yeye akishapanga nioe muda flani na mwanamke nikishampata basi nitaoa, lakini naweza kutaka kuoa nikakaa muda mchache na huyo mwanamke kwahiyo vuteni subira muda ukifika nitaoa ndugu zangu.


 MC CHINGA DODOMA FM:- Ule wimbo wako wa chozi la mnyonge unaonekana kama kuna mtu alikukwaza ukaamua kutunga je ni kweli?.


  HASSAN ALLY:- Dada angu mc chinga ni kwamba ule wimbo chozi la mnyonge nimezungumzia maisha yangu binafsi na maisha ya wengine kwasababu wengi huwa wanalia kwasababu ya kudhulumiwa haki zao, nilikuwa nataka kuwaambia tu kwamba mwenyezimungu anatazama sana chozi la mnyonge.


KAKA ZEMA CITIZEN KENYA:- Mimi nakupongeza ila naomba kuuliza kuna baadhi ya maneno huwa unayatumia kwenye nyimbo zako mfano kinyama kidogo...wanawake wainame...wanaume wasimame! maneno hayo huoni kuwa yakitafsiriwa vibaya ni matusi makubwa?.


 HASSAN ALLY:- Kaka zema kuhusu hayo maneno ambayo unayazungumza kweli ni maneno ya mafumbo yaani mafumbo kwenye taarab yanapendeza sana mtu akitafsiri neno kama hilo mtu mzima anakuwa ametafsiri na lilikuwa limefichwa hivyo mtoto mdogo hawezi kutafsiri, mbaya kutoa maneno wazi wazi.


           Maswali yalikuwa ni mengi sana toka kwa watangazaji labda ni vyema japo nikaorodhesha baadhi ya majina ya watangazaji waliopata bahati ya kumuuliza maswali young hassan ally wa kwanza ni Hotie kutokea generation fm mbeya, Rachel wa pamoja fm mpanda, malick shakhran wa hits fm zanzibar, Asha simba wa kilosa fm kilosa morogoro, Warda chande wa passion fm dar, Asha athuman wa mbeya fm, Diva wa hits fm zanzibar, Sauda mkalokota wa zenji fm zanzibar, Devota sotele wa passion fm mwanza, Lui wa moshi fm mkoani kilimanjaro, koleta wa redio free africa mwanza, Grace wa sauti fm mwanza tanzania, Bobo mautundu wa mlimani redio dar, Edna wa Afm dodoma, Nadrah wa dream's fm mbeya na wengineo wengi sana, mtanisamehe wale ambao sikubahatika kuwataja hapa.....JUMATATU IJAYO KATIKA SAGMENT YETU YA "KIKAANGONI"  TUTAKUWA NAE MALKIA WA MIPASHO NCHINI TANZANIA BIBIE KHADIJA OMARY KOPA, ATAJIBU MASWALI YENU NA MUDA NI ULE ULE MSIKOSE...NAWAPENDA SANA!!.


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni