TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 22 Aprili 2016

AISHA VUVUZELA USO KWA USO NA WATANGAZAJI ZAIDI YA 95 WA TAARAB KATIKA KIKAANGONI WIKI HII

NA KAIS MUSSA KAIS.


AISHA OTHMAN VUVUZELA.

           Baada ya wiki iliyopita kuwa na khadija yusuph wa jahazi modern taarab katika kile kipengele chetu matata cha "kikaangoni wiki hii", basi jumatatu ijayo yaani tarehe 25/4/2016 tutakuwa nae Aisha othman vuvuzela msanii aliejiunga jahazi akitokea wakaliwao modern taradance.


       Akithibitisha kuwepo katika kipengele hicho Aisha alijirekodi "voice note" na kuwatumia watangazaji ndani ya group hilo na pia aliwaambia wandishi wa mtandao huu katika dawati lao kuwa atatoa ushirikiano mkubwa sana siku hiyo ya jumatatu panapo majaliwa yake mwenyezimungu. watangazaji walimpendekeza vuvuzela awepo katika kipengele hiki ukizingatia wana mengi sana ambayo wanataka kujua toka kwake, hivyo naamini jumatatu ndani ya group la watangazaji kutapendeza sana.


        Kipengele hiki kimekuwa kikijizolea umaarufu mkubwa kila siku zinavyokwenda kwa sababu wapenzi na wadau wamekuwa wakijua mambo mengi sana yaliyofichika toka kwa wasanii kulingana na maswali ambayo wamekuwa wakiyauliza watangazaji hao, tukutane tena hapa wiki ijayo kwa maswali na majibu kati ya Aisha othman vuvuzela na watangazaji hao!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni