TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 22 Aprili 2016

HARAKATI ZA UBUYU WA TAARAB NA KAIS MUSSA KAIS NDANI YA EBONY FM KILA SIKU YA JUMAPILI...USIKOSE!.

NA MWANDISHI WAKO.


          Katika kile kinachoonekana kukubalika kwa kazi anayoifanya kais mussa kais ambae ni mkurugenzi wa mtandao huu, uongozi wa redio ebony fm yenye maskani yake nyanda za juu kusini mkoani iringa wamempa nafasi ya kufanya yake katika kipindi cha taarab kiitwacho "kwa raha zote" kinachoongozwa na Tinna Tanna!.


     Kipindi hicho ambacho huwa kinakuwa kila siku za jumamosi na jumapili kuanzia saa saba mchana hadi saa tisa alasiri chini ya mtangazaji huyo Tinna tanna. kais mussa kais atakuwa akipatikana kila siku ya jumapili na jina la kipengele atakachokuwa anakiongoza kitaitwa "Harakati za ubuyu wa taarab na kais mussa kais", humo watahusika zaidi wasanii wa taarab kwa kufanya mahojiano yatakayo pelekea wewe msikilizaji kumtambua zaidi msanii husika na mwisho huwa kunakuwa na swali la kizushi ambalo msanii atatakiwa kujibu.


     Kuanzia jumapili hii ya tarehe 24/4/2016 kipengele hicho kitaanza kuruka hewani rasmi, kwahiyo ukiwa mdau wa taarab unaombwa kuendelea kusikiliza ebony fm ili ujue je ni msanii gani au wasanii gani ambao kais mussa kais ataanza nao!, tuendelee kumpa sapoti na penye mapungufu ruksa kukosoa ukiwa kama mdau ila busara na nidhamu inabidi zitumike.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni