TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 22 Aprili 2016

UTAMBULISHO WA AISHA VUVUZELA NA ZUBEDA MLAMALI, JAHAZI MODERN TAARAB YASHUSHA KIINGILIO.

NA KAIS MUSSA KAIS.


       Bendi ya jahazi modern taarab yenye maskani yake jijini dar es salaam leo kupitia kwa mkurugenzi wake mfalme mzee yusuph ametoa tamko la kushusha kiingilio cha show yao ya utambulisho wa wasanii wake wapya zubeda mlamali na aisha vuvuzela siku ya jumapili ya tarehe 1/5/2016 toka elfu 10,000/= mpaka elfu 8,000/= za kitanzania.


      Akifafanua zaidi jambo hili mfalme mzee yusuph alisema kwamba ameamua kushusha kiingilio ili wapenzi wa jahazi modern taarab wajitokeze kwa wingi, na pia nimewathamini sana wadau wangu kwani hiyo elfu mbili ambayo nimeipunguza hapo inaweza kumsaidia shabiki wangu kwa mambo mengine.kikubwa nawaomba wadau waje kwa wingi kwani siku hiyo itakuwa ni tofauti na siku zingine.


     Ikumbukwe kuwa ni jana tu bendi hii ya jahazi modern taarab ilitangaza kuwa kiingilio katika show hiyo kitakuwa ni shilingi elfu kumi lakini leo hii mfalme mzee yusuph kwa kuonyesha kuwa anawajali na kuwathamini wapenzi wa bendi yake ya jahazi ameamua kupunguza kiingilio, hongera sana mzee yusuph kwa ulichokiamua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni