TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 24 Aprili 2016

ZUBEDA MLAMALI AAHIDI KUFANYA MAKUBWA TAREHE 1/5/2016 PALE TRAVETINE MAGOMENI...USIKOSE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


ZUBEDA MLAMALI AKIWA STEJINI.

          Jina la zubeda mlamali sio geni miongoni mwa majina ya waimbaji wa taarab nchini tanzania, kwa sasa anapatikana katika bendi ya jahazi modern taarab chini ya mkurugenzi wake mfalme mzee yusuph.


         Siku ya tarehe 1/5/2016 ndani ya ukumbi wa travetine magomeni jijini dar kutakuwa na bonge la show toka kwao jahazi modern taarab na ni maalum kwa utambulisho wa wasanii wapya ambao wamejiunga na bendi hiyo akiwemo zubeda mlamali na aisha vuvuzela. akizungumza na mtandao huu makini zubeda mlamali alisema kwamba amepania kufanya makubwa katika show hiyo maalum ya utambulisho.


      Nitakuwa mpya siku hiyo kwani kiu yangu ya kujiunga na jahazi ambayo nilikuwa nayo kwa kipindi kirefu hatimae imetimia rasmi, jahazi modern taarab ni bendi bora sana na kila msanii anapenda sana awepo kundini, kikubwa nawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi siku hiyo ya tarehe 1/5/2016 katika ukumbi wa travetine magomeni kwa kiingilio cha shilingi 8,000/= tu alimaliza kwa kusema!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni