TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 21 Aprili 2016

PRINCE BLACK KOPA KUINGIA STEJINI SIKU YA UZINDUZI TAREHE 7/5/2016 DAR LIVE KWA STYLE YAKE TOFAUTI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Muimbaji chipukizi na anaekuja kwa kasi ya ajabu Black kopa ambae ni mtoto wa malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa, amesema anataka kufanya tofauti juu ya aina ya uingiaji wake stejini siku ya uzinduzi wa bendi ya ogopa kopa sambamba na uzinduzi wa albam mpya pale dar live tarehe 7/5/2016.

 

PRINCE BLACK KOPA AKIWA STEJI.

       Akiongea na mwandishi wa habari hizi black kopa alisema kuwa siku ya uzinduzi wa albam ya wakaliwao pale dar live niliingia kama mtoto wa mfalme huku nikilindwa na walinzi wa jumba la mfalme hali iliyowafanya wapenzi na wadau kunipa hongera sana kwa ubunifu wangu.sasa katika uzinduzi wa bendi yangu itakuwa ni zaidi ya vile kikubwa nawaomba wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya tarehe 7/5/2016 kwani hata malkia kuna kitu special atafanya kwa ajili ya wapenzi wa taarab watakaofika siku hiyo.

 

        Mtandao huu unawapongeza sana ogopa kopa kwa maandalizi mazuri ambayo wamekuwa wakiyafanya karibu kila siku katika kuelekea siku hiyo ya uzinduzi ndani ya dar live, tunawaomba wadau wajitokeze kwa wingi siku hiyo ya uzinduzi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni