TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 21 Aprili 2016

ALJAZEERA WAAHIDI BURUDANI BAB-KUBWA JUMAMOSI HII NDANI YA UKUMBI WA D.D.C. KARIAKOO...USIKOSE!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


        Unapozungumzia bendi inayofanya vizuri kwa sasa katika miondoko ya "old is gold taarab" ni lazima uitaje aljazeera modern taarab bendi yenye maskani yake kariakoo jijini dar es salaam.


     Bendi hii ambayo hufanya show zake katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo jijini dar es salaam kila siku ya jumamosi, leo viongozi wake Hamisi chizi na Abuu mgeni wamefika katika ofisi zetu na kujinasibu kwamba jumamosi ijayo yaani tarehe 23/4/2016 wamewaandalia wapenzi wao burudani ya nguvu kwani kwa kipindi kirefu sana wasanii wao wapo kambini wakijifua kwa kufanyia mazoezi nyimbo nzuri ambazo zitawaburudisha na kukata kiu ya wapenzi wao.


     Mimi nawaomba kujitokeza kwa wingi ili kuja kujionea ubora wa bendi yao kwa sasa kutokana na kuongeza waimbaji wapya na wapiga vyombo wapya kabisa, wakati huo huo mkurugenzi wa bendi hiyo Jamali mpera mpera amewaahidi wapenzi watakaotaka shisha basi watapata bure kabisa bila kulipa pesa yoyote...hao ndio aljazeera modern taarab wataalam wa old is gold taarab kwa sasa hapa jijini dar nenda ukawaone na upate burudani uliyoimiss kwa muda mrefu, kumbuka ni katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni