TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 21 Aprili 2016

JAHAZI MODERN TAARAB KUWATAMBULISHA RASMI AISHA VUVUZELA NA ZUBEDA MLAMALI TAREHE 1/5/2016 NDANI YA TRAVETINE MAGOMENI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

          Habari ya mjini kwa sasa ni usajili wa nguvu uliofanywa na bendi ya jahazi modern taarab kwa kuwachukuwa waimbaji wawili Aisha vuvuzela na Zubeda mlamali kutoka bendi mbili tofauti, wakati zubeda mlamali anatokea east african melody nae Aisha vuvuzela anatokea wakaliwao modern taradance.

 

     Uongozi wa bendi hiyo chini ya viongozi watendaji Hamisi boha, Seif shiboli na Awadh wameandaa show bab-kubwa kwa ajili ya kuwatambulisha rasmi ndani ya bendi hiyo waimbaji hao siku ya jumapili tarehe 1/5/2016 pale katika ukumbi wao wa nyumbani wa travetine magomeni jijini dar es salaam.

 

    Hamisi boha alisema kwamba siku hiyo wasanii hao watatambulisha nyimbo zao mpya kabisa ndani ya bendi hiyo na kutakuwa na ma-surprise kibao kutoka kwa kampuni yao ya jahazi entertainment chini yake mfalme mzee yusuph moja wapo ni watu mia moja wa mwanzo kuingia katika ukumbi huo watapata t-shirt za jahazi modern taarab, kiingilio katika onyesho hilo ni shilingi elfu kumi 10,000/= kwa kila mmoja na milango itakuwa wazi kuanzia saa moja huku show kamili ikianza saa mbili kamili, uongozi wa jahazi umewaomba wadau na wapenzi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kujionea vipaji toka jahazi modern taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni