TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 19 Aprili 2016

ABUU MGENI:- ALJAZEERA MODERN TAARAB SISI NI KAZI TU, NA WATAISOMA NAMBA MWAKA HUU.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Director wa bendi ya aljazeera modern taarab Abubakar mgeni almaarufu Abuu mgeni leo amejinasibu mbele ya wandishi wa mtandao huu kuwa wamepania kufanya makubwa sana ili kuleta burudani nzuri kwa mashabiki wa taarab ya "old is gold".


ABUU MGENI-DIRECTOR WA ALJAZEERA.

       Akizungumza kwa kujiamini Abuu mgeni alisema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kwa asilimia themanini kukamata soko la muziki huu hapa jijini dar es salaam, na hili linajidhihirisha katika maonyesho yao pale katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo kwani wapenzi wamekuwa wakiongezeka na kusifia kile kinachofanyika na vijana wa aljazeera modern taarab.


    Tulipoamua kufanya mabadiliko kwa kurekodi nyimbo zetu mpya na kuzipeleka redioni kuna baadhi ya watu walitubeza na kusema kamwe hatutofanikiwa, lakini leo hii sura zimewashuka kwa aibu na nasikia wapo wanaanda nyimbo mpya na wao!, mimi nasema na bado wataendelea kuiga kila tunachofanya wakumbuke kuwa hii ndio aljazeera watoto wa town, hapa kwetu kazi tu na mwaka huu wataisoma namba alimaliza kwa kusema director huyo asie na majivuno.


        Ikumbukwe bendi hii ya aljazeera modern taarab huwa wanafanya show zao pale katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo kila jumamosi na wamekuwa wakifanya vyema kulingana na maoni ya wapenzi na mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni