TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 19 Aprili 2016

KHADIJA YUSUPH:-NIMEMSALIMIA LEYLA ZAIDI YA MARA TATU TUMALIZE TOFAUTI ZETU KAKAA KIMYA, NAMI SASA NIPO KIMYA

NA KAIS MUSSA KAIS.


KHADIJA YUSUPH-SAUTI YA CHIRIKU ORIGINAL.

               Ilikuwa ni jumatatu tulivu kabisa iliyoambatana na mvua za hapa na pale katika jiji la dar es salaam, ndipo kile kipengele kinachoendelea kujizolea umaarufu "kikaangoni wiki hii" ndani ya group la whatsap la watangazaji wa taarab kilipokuwa kikiendelea kwa maswali na majibu chini ya mgeni wetu khadija yusuph tokea jahazi modern taarab.

 


      Saa moja na dakika tano usiku ndipo khadija yusuph nilipomuunganisha "live" na watangazaji hao na maswali kuanza kama ifuatavyo:-

 


KAKA ZEMA CITIZEN REDIO KENYA:- Umekuwa katika tasnia hii ya kwa muda mrefu sana kabla wengi wetu hapa hatuja fikilia kuwa watangazaji, siri ya sauti yako kutochuja ama kuzeeka ni nini? na je wazungumziaje taarab kwa sasa na wakati ule wa nyuma?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Kwakweli sauti yangu mimi situmii kitu chochote kile, sauti hii ni original kama wanavyoniita sauti ya chiriku original na sauti yangu ilivyo ndio hivi hivi siyumi kitu chochote kile kusema nakula hiki au kile nipo tu kawaida hiki ni kipaji kimetoka kwa mama angu mwanajuma mzee, maana mama yeye alikuwa ni muimbaji wa culture music club.

 


SHUFAA WA KAYA FM BAGAMOYO:- Nini malengo yako baada ya mgogoro ambao upo kati yako na wifi yako, je utaendelea kufanya kazi na kaka yako katika jahazi au utaondoka kwenda bendi ingine?, tuambie maendeleo ya jahazi modern taarab baada ya sintofahamu ambayo ilitokea na vipi mahusiano yako nje ya kazi na kaka yako ni sawa na mwanzo au kuna tofauti yoyote unaiona?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Mahusiano yangu na kaka angu mzee yusuph yapo kama kawaida na naona yameongezeka zaidi kuwa mazuri kwa sasa, na malengo yangu kwa hizo sintofahamu zilizotokea kamwe siwezi kuacha jahazi kwa sababu ya maneno ya waja, hao wamezoea kusema ni kawaida tu mimi bado nipo jahazi na nitaendelea kuwa jahazi kama kawaida.

 


MALICK HITS FM ZANZIBAR:- Mimi ningependa kujua ukiacha kuimba unatarajia kufanya nini?, vile vile khadija yusuph unavuma sana kuwa unapenda sana wanaume wadogo yaani "ndogo ndogo" sio wa type yako na pia ukiolewa hukai kwa mume yaani "ndoani" hivi ni kweli au ni uvumi tu wa watu?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Mimi nikiolewa na kaa kwenye ndoa, hakuna ndoa ambayo nimeolewa nikakaa siku mbili siku tatu nikaachwa, na sipendi ndogo ndogo mume wangu wa kwanza alienioa kanizidi umri tena kanizidi sana, mume wangu wa pili ndio kabisaaa! tena simpati hata kidogo wote yaani siwapati, sema mume wangu huyu ndio umri wetu ni mmoja na sio mdogo, nilivyo mimi na yeye yupo hivyo hivyo mwaka niliozaliwa mimi na yeye kazaliwa mwaka huo huo si mdogo ila mimi naonekana mkubwa sababu ya unene tu nilionao lakini mimi mdogo tu kiumri nimezaliwa mwaka 1980.

 


SALMA WA MAISHA FM DODOMA:- Ningependa kujua kutoka kwa khadija yusuph, hivi umeshawahi kujuta tokea uingie katika fani hii ya taarab?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Nishawahi kujuta na mpaka hapa nilipo najutaa!!, na kikubwa ni huu ugomvi uliokuwa ukiendelea maana iliingizwa mpaka familia yangu, mama yangu katukanwa sana nimelia sana kwa matusi yale, kwakweli najuta kuwepo humu katika taarab!.

 


EDNA AFM DODOMA:- Mimi nionavyo mhimilimkubwa wa bendi ya jahazi modern taarab ni wewe, mzee yusuph na leyla rashid sasa huoni kuwa unawaga mashabiki zako kwa mgogoro huo na wifi yako?, vile vile unaonekana unampenda sana mke mdogo chiku kuliko leyla binafsi naona si vyema hivi unaweza kuniambia ni kwanini uligombana na leyla?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Kwakweli mimi siwezi kuwagawa mashabiki, ila anaenifahamu vizuri basi ananijua tokea huko nilivyoanza kuimba sikuwa na tabia kama hizi ila haya yametokea kwa sasa na hii yote naona kwa sababu tupo pamoja katika bendi lakini labda ningekuwa nipo sehemu ingine nafikiri yasingeweza kutokea haya yote, na simpendi mke mdogo sana eti mke mkubwa namchukia mimi nawapenda wote ila haya mambo ya ukewenza mtu mwingine anaeelewa anaelewa na asieelewa haelewi kwasababu ukewenza hakuanza yeye leyla wameanza mabibi zetu na mababu hata mimi mwenyewe nilikaa ukewenza lakini sikugombana na wifi yangu wala kugombana na mkwe wangu kwasababu ukewenza ni mume, kama mume hayupo vizuri hapo ndipokunakuwa na tofauti lakini si wifi wala mkwe.

 


UMMY AMEIR SWAHIBA FM ZANZIBAR:- Unazikabiri vipi changamoto unazokutana nazo katika muziki huu wa taarab, pia ni kwanini unawapa nafasi mafitina ambao wanaingilia kati kukuchonganisha wewe na wifi yako leyla rashid ukizingatia wewe na leyla sasa ni familia moja.

 


KHADIJA YUSUPH:- Hakuna mafitina wowote ambao wanatuchonganisha hilo nakataa nasema kiroho safi, mimi ninavyojua leyla amenuna mwenyewe nimemsalimia zaidi ya mara tatu amekataa kuitikia, basi na ndio mpaka leo ipo hivyo hivyo hanisalimii simsalimii hakuna fitina hakuna nani fitina labda yeye mwenyewe na hata kama yupo katika familia kweli, sawa na mimi sijamkataa kwasababu mimi ningemkataa basi hata ile siku ya mwanzo aliyoenda kuolewa na mimi ndio nilikuwepo katika familia hakuwepo mtu yeyote nilikuwa peke yangu.

 


DAZINA DODOMA:- Khadija inasemekana tokea leyla amejifungua mwanawe hujakwenda kumuona je jambo hili lina ukweli wowote?, na hivi unafikili ni sawa mtoto kuingizwa katika ugomvi wenu kwakuwa naamini huyu ni mtoto wako pia?.

 


KHADIJA YUSUPH:- Ni kweli tokea mtoto kazaliwa sijawahi kumuona na mpaka leo hii sijamuona kabisa, na si mtoto tu katika huu ugomvi kaingizwa mama yangu mzazi, kaka angu ambae ni mlemavu kaingizwa hajui moja wala mbili kinachoendelea, baba yangu pia ameingizwa sio mtoto tu hata hawa wazee wangu hayahusu na sio sawa kuingizwa.

 


        Maswali yalikuwa mengi sana kama ilivyo kawaida ya kipengele hiki lakini haya ni machache sana zaidi ya sana, mwisho kabisa khadija alitoa lile lake la rohoni kwa kusema kuwa anaumizwa sana na yale matusi yaliyopita ndio yana muuma sana yememfanya atoe machozi yake kwa ajili ya matusi tu ya waja, watangazaji baadhi ambao nao walipata nafasi ya kuuliza maswali lakini sikubahatika kuyaorodhesha maswali yao hapa ni sauda mkalokota wa zenji fm,nadya omary wa bomba fm, aisha mbegu wa times fm, tinner tunner wa ebony fm, maria wa kwizera fm ngara, blandina wa tk fm tanga, Tuma wa hits fm, asha wa victoria fm musoma, afarah wa safari fm mtwara na wengineo wengi, tukutane tena wiki ijayo katika kipengele hiki...Ahsanteni sana!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni