TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 17 Aprili 2016

MZEE YUSUPH:- AISHA WA JAHAZI MODERN TAARAB HAWEZI KUITWA VUVUZELA, NITAMBADILISHA JINA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Katika kile kinachoonekana nyota ya muimbaji aisha vuvuzela kung'aa, mfalme mzee yusuph ambae ni mkurugenzi wa bendi ya jahazi modern taarab amesema kwamba anataka kumbadilisha jina aisha vuvuzela kwani jina hili tafsiri yake ni kupiga kelele.

AISHA OTHMAN VUVUZELA.


       Mimi nitamtafutia jina zuri sana na litakuwa bab-kubwa kulingana na uwezo wake katika uimbaji, sipendi kumuita vuvuzela au kusikia akiitwa hivyo! linamshushia heshima yake. ndugu mwandishi, mimi ni bingwa wa kuwatengeneza wasanii wakaja kufahamika. Aisha ni muimbaji mzuri na anafit kuwa hapa jahazi ila jina alilopewa ndio tatizo, nakuahidi nitambadili jina hivi karibuni.


     Alipoulizwa ni jina lipi unafikilia kumpatia? alijibu kuwa ni mapema sana ukizingatia ni leo tu ameanza kazi rasmi hapa jahazi, vuta subira kwani kila kitu kitakuwa sawa wakati ukifika. Aisha vuvuzela ambae anatamba na wimbo ukinuna uwe na sababu ambao aliuimbia wakati yupo wakaliwao modern taradance kwa sasa amebadili upepo na kuamua kujiunga na jahazi modern taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni