TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 17 Aprili 2016

AISHA VUVUZELA NA ZUBEDA MLAMALI WAJIUNGA NA JAHAZI MODERN TAARAB NA KUANZA KAZI RASMI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Bendi ya jahazi modern taarab imeendelea kujiimarisha katika safu yake ya waimbaji baada ya kuongeza waimbaji wawili aisha othman vuvuzela tokea wakaliwao modern taradance na zubeda mlamali tokea east african melody.


AISHA OTHMAN VUVUZELA.

        Dawati la habari la mtandao huu lilipopata nyeti hizo bila hiyana wala fuvu tete! tulisogea mpaka pale travetine magomeni ambapo jahazi huwa wanafanya show kila jumapili, nia ni kuthibitisha taarifa hizi na pia kuzungumza na mfalme mzee yusuph ambae ndie mkurugenzi wa bendi hii.


      Tuliingia katika ukumbi wa travetine magomeni muda wa saa sita na dakika saba usiku na moja kwa moja macho yalielekea katika steji ya jahazi ili kuhakikisha ni kweli wasanii hao wapo au maneno ya walimwengu tu!, ndipo tulipojiridhisha baada ya kuwaona wote wawili wakiwa steji wanawajibika, kilichofuata ni kumtafuta mkurugenzi wa jahazi mzee yusuph na alipopatikana haya ndiyo aliyoyasema:-

ZUBEDA MLAMALI.

 

       Ni kweli nimeamua kuwachukua aisha vuvuzela na zubeda mlamali ili kuongeza nguvu katika kikosi changu, lakini pia uwezo mkubwa wa waimbaji hawa nao naweza kusema umenishawishi kuwachukua ndani ya jahazi modern taarab, kwa sasa wasanii hawa wataendelea kuwepo hapa jahazi na mungu akipenda katika album ijayo naweza kuwapa nyimbo mpya lakini yote itategemea nidhamu na utendaji mzuri wa kazi zao alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni