TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 16 Aprili 2016

USIKOSE KUMSIKILIZA AISHA MBEGU "SAUTI YA NINGA" LEO JUMAPILI NDANI YA TIKISIKA KIPWANI 100.5 TIMES FM.

NA KAIS MUSSA KAIS.


         Aisha mbegu au ukipenda unaweza kumuita "sauti ya ninga" leo jumapili rasmi anaanza kutangaza kipindi cha taarab kiitwacho tikisika kipwani ndani ya times fm 100.5 kuanzia saa mbili usiku mpaka saa nne kamili usiku.


        Akizungumza na mtandao wa ubuyu wa taarab Aisha alisema kuwa kipindi chake anataka kukifanya kiwe tofauti kidogo maana amepanga kuzipa kipaumbele zile bendi ambazo zimekuwa hazisikiki lakini zimesharekodi nyimbo zao!, kuna mambo mengi sana nimepanga kufanya ili kuboresha kipindi changu ila kwa kuanza leo jumapili nitakuwa na mahojiano na bendi ya aljazeera modern taarab bendi yenye maskani yake kariakoo jijini dar.


     Aisha aliendelea kuzungumza kuwa wadau na wapenzi wa taarab kuna kitu kikubwa amepanga kuwafanyia hivyo amewaomba kumpa sapoti nae kamwe hatowaangusha, amewataka wasikilizaji wasisite kutoa maoni yao juu ya kipindi chake hicho kwani nia ni kujenga na kuboresha zaidi kupitia wasikilizaji alimaliza kwa kusema, ikumbukwe kuwa Aisha mbegu kabla ya kurejea tena redio times alikuwa katika kituo cha redio cha Efm 93.7 ambacho nacho kipo hapa jijini dar. Haya shime wadau na wasikilizaji tusikose kumsikiliza aisha mbegu ndani ya redio times itakapofika saa mbili kamili na leo atakuwa na vijana wa aljazeera modern taarab live studio wakitambulisha nyimbo zao mpya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni