TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 29 Aprili 2016

ALJAZEERA MODERN TAARAB "OLD IS GOLD TAARAB" LEO JUMAMOSI WAPO D.D.C. KARIAKOO NJOO UPATE BURUDANI.

NA KAIS MUSSA KAIS.
 

             Ile siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa taarab asilia "old is gold" hatimae imefika ni leo hii jumamosi ndani ya ukumbi tulivu wa D.D.C. kariakoo jijini dar es salaam, vijana wako wa aljazeera modern taarab watashusha burudani maridadi kabisa ambayo haitokuchosha kabisa.


       Akizungumza na mtandao huu Hamisi chizi ambae ndio director msaidizi wa bendi hiyo alisema kuwa waimbaji wake wamejipanga vyema kufanya makamuzi ya nguvu kama kawaida yao, na leo kuna nyimbo ambazo wamezifanyia mazoezi watazipiga kwa mara ya kwanza, nyimbo hizo hazijawahi kupigwa na bendi yoyote ile hapa dar es salaam. unajua ndugu mwandishi kuna nyimbo nyingi sana za old is gold na nzuri sana lakini bendi nyingi za hapa zinang'ang'ania kibali, sio mimi na nyinginezo za kawaida.

     Mimi nawaomba wajitokeze kwa wingi leo wajionee vijana wa aljazeera ni vitu gani tumeviandaa kwa ajili yao alimaliza kwa kusema, Vijana hawa wa aljazeera huwa wanafanya show zao katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo kila siku ya jumamosi kwa kiingilio cha shilingi elfu sita tu!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni