TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 29 Aprili 2016

UZINDUZI WA OGOPA KOPA DAR LIVE MBAGALA, WAGENI MBALIMBALI TOKA NJE YA NCHI WAANZA KUMIMINIKA TANZANIA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


       Joto la uzinduzi wa bendi ya ogopa kopa classic limeanza kupanda kwa kasi ya ajabu baada ya wageni mbalimbali kuanza kuingia nchini wakitokea nchi mbalimbali tayari kwa onyesho hilo bab-kubwa ambalo linatarajia kufanyika tarehe 7/5/2016 ndani ya ukumbi wa Dar live mbagala jijini dar es salaam.


     Shaymaa abubakar ni raia wa comoro ambae tayari ameingia tanzania akiwa na kampani yake ya watu nane maalum kabisa kwa uzinduzi huo wa bendi sambamba na albam mpya, mwanamke huyu alipata taarifa za uzinduzi wa ogopa kopa classic bendi kupitia mtandao wa ubuyu wa taarab ambao unafanya vizuri sana nchini comoro, akawa anafanya mawasiliano mara kwa mara na dawati letu la habari na kuahidi kuwa atakuja tanzania akiwa na kampani yake nzima, hawa ni mashabiki wakubwa wa khadija kopa.


     Wakati huo huo vyombo vya habari kutoka kenya nikimaanisha citizen redio, bahari fm, pilipili fm na KBC nairobi zote kwa pamoja wametuma watangazaji wao kuja hapa tanzania kuripoti tukio zima la uzinduzi wa bendi hii ya ogopa kopa, watangazaji ambao watakuja tokea kenya ni kaka zema, salim barissa, mamaa madikodiko na Aisha saggaf. ikumbukwe katika show hiyo bendi ambazo zitasindikiza uzinduzi huo ni jahazi modern taarab, wakaliwao modern taradance, yamoto bendi na msagasumu au ukipenda muite Rais wa uswazi. show itaanza saa mbili kamili usiku na kiingilio ni shilingi elfu 10,000/= nyote mnakaribishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni