TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 28 Aprili 2016

TETESI:- MUSSA MIPANGO KURUDI TENA JAHAZI MODERN TAARAB?.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MUSSA MIPANGO AKIWA KATIKA STEJI YA JAHAZI MODERN TAARAB.

           Mpiga gita la besi mwenye umaarufu mkubwa katika muziki huu wa taarab nchini tanzania mussa mipango almaarufu mussa mussa inasemekana yupo katika mipango ya kurudi tena katika bendi yake ya zamani jahazi modern taarab.


        Habari zilizotufikia kwenye dawati letu zinasema kuwa kuna mambo yapo nyuma ya pazia kuhusu kurudi tena ndani ya bendi hiyo kwa mussa mipango. kama ilivyo ada ya mtandao huu tulifanya kila liwezekanalo kuweza kukutana na uongozi wa jahazi modern taarab ili waweze kuweka wazi suala hili na alipopatikana Hamisi boha ambae ni mmoja wa viongozi wa juu wa bendi hiyo yeye alikuwa na haya ya kusema.


       Mussa mipango amekuwa akija katika baadhi ya show zetu na hii ni kawaida kwa wasanii kutembeleana, sio mussa tu wasanii wa bendi mbalimbali wamekuwa wakija na kupiga chombo chochote ambacho anaweza na ndivyo alivyofanya mussa! kuhusu yeye kurudi ndani ya jahazi modern taarab inawezekana na halina shida hilo ila ni mapema sana kulizungumzia ndugu mwandishi.


      Mtandao huu ulipomtafuta mussa mipango nae ili azungumzie jambo hili yeye alisema sina la kuzungumza juu ya hilo kwa ushauri tuu unaweza kuwauliza viongozi wa jahazi modern taarab labda watakuwa na lolote la kukujibu. Sisi kama uongozi mzima wa mtandao huu wa ubuyu wa taarab tunasema sio mbaya kwa mussa mipango kurudi tena kundini kwani umuhimu wa mussa mipango ndani ya jahazi modern taarab unafahamika wazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni