TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 27 Aprili 2016

PRINCE BLACK KOPA USO KWA USO NA WATANGAZAJI WA TAARAB AFRIKA MASHARIKI NDANI YA KIKAANGO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


PRINCE BLACK KOPA.

           Watangazaji wa taarab ndani ya group la whatsap la ubuyu wa taarab hatimae jumatatu ijayo watamuweka kati prince black kopa kwa maswali kadha wa kadha kwani kuna mengi sana yamepita hapa kati yanayomuhusu msanii huyu.


       Watangazaji wamekuwa na utaratibu wa kupiga kura ya wazi na wakati mwingine kura ya siri kulingana na mazingira ili kumchagua msanii ambae wao wanamuhitaji awepo ndani ya kikaango kwa siku hiyo ya jumatatu, taarifa zilipomfikia prince black kopa kwamba watangazaji wamemchagua yeye kuwepo ndani ya kikaango kwa jumatatu ijayo, kwanza alishtuka sana na kutaka kukataa lakini alipotajiwa idadi ya watangazaji ambao wapo katika group na wangapi ambao wamempendekeza yeye kuwepo kikaangoni alikubali.


     Hivyo basi nikiwa kama admin wa group hilo la watangazaji wa taarab afrika mashariki napenda nimtangaze rasmi kuwa jumatatu tutakuwa nae prince black kopa katika ule utaratibu wetu wa kawaida katika kuuliza na kujibu maswali, tungoje ni nini kitatokea siku hiyo. Mahojiano ya Aisha othman vuvuzela na watangazaji nitayaweka humu muda mchache ujao unataka kujua vuvuzela alizungumza nini?, basi kuwa nami baadae kidogo hapa hapa ubuyu wa taarab...Thanx!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni