TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 27 Aprili 2016

JAHAZI KOLOMBWE MODERN TAARAB KUAZIMISHA BIRTHDAY YAO LEO NDANI YA SCOPION PUB MBAGALA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


JAHAZI KOLOMBWE MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI.

           Bendi ya jahazi kolombwe modern taarab siku ya leo jumatano inatarajia kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa scopion pub mbagala charambe kwa mbiku.


      Akizungumza na mtandao huu bora wa taarab nchini mkurugenzi wa bendi hiyo Babu chollo alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na pia amewataka wasanii wote ambao waliwahi kuwepo katika bendi hiyo kipindi cha nyuma basi waje tukate keki kwa pamoja!. leo kutakuwa na ma-surprise kibao toka kwa uongozi wa jahazi kolombwe n wasanii wetu wamejipanga vyema kuwapa burudani wapenzi wetu.


     Jahazi kolombwe modern taarab kuna A na B lakini kwakuwa leo ni siku maalum kwetu basi bendi zote mbili zitaungana na wadau wetu katika kusherehekea, kikubwa tunaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi kwani show itaanza saa moja kamili usiku na kumalizika saa sita usiku alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni