TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 26 Aprili 2016

MISS TURIPLETY:- ALJAZEERA MODERN TAARAB NIMEVUTIWA SANA NA SHOW ZAO ZA D.D.C KARIAKOO.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MISS TURIPLETY.

           Mfanyabiashara wakike ambae huwa anafanya biashara zake kati ya oman na hapa tanzania miss turiplety kama anavyofahamika na wengi, siku ya jumamosi iliyopita ndani ya ukumbi wa D.D.C. kariakoo alizungumza na mwandishi wa habari hizi na kutoa pongezi kubwa kwa bendi ya aljazeera kutokana na kuvutiwa na burudani zake.


       Akizungumza kwa tabasamu kubwa Turiplety alisema kuwa aljazeera wana vigezo vyote vya kuwa bendi bora ya old is gold hapa dar es salaam kwa sababu wanajitambua sana, waimbaji wao wapo smart, wapiga vyombo wao wote wamevaa sare, nyimbo wanazopiga ni vigumu kuzisikia bendi ingine yoyote ambayo wanapiga kopi za old is gold, wana nidhamu ya kazi na mwisho huu ukumbi ambao wanafanyia show zao upo sehemu tulivu na ni msafi sana, kwa yeyote ambae anatokea oman au nchi nyingine kama mimi sehemu kama hii ni lazima aipende niamini niyasemayo ndugu mwandishi.


      Mimi natarajia kusafiri kurudi tena oman siku ya jumatano tarehe 4/5/2016 na nitakuwa balozi mzuri wa kuitangaza aljazeera huko niendako, kikubwa nawaomba wasilewe sifa wazidishe juhudi na mafanikio watayaona zaidi katika siku za usoni alimaliza kwa kusema. Ikumbukwe kuwa bendi ya aljazeera huwa inafanya show zake katika ukumbi huo wa D.D.C. kariakoo kila siku ya jumamosi kwa kiingilio cha shilingi elfu 6,000/= za kitanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni