TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 24 Aprili 2016

HIZI NDIZO SHOW TANO TAKATIFU KABISA KWA WIKI ZA G FIVE MODERN TAARAB, ZISOME HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MUSSA KIJOTI AKIKAMUA NDANI YA JUKWAA LA G5!.

         Bendi yako ya G five modern taarab chini ya mkurugenzi wakeHamisi slim au mzee wa "manyamnyam" leo hii imetangaza rasmi show zake tano kwa wiki ambazo zitakuwa zikilindima katika kumbi mbalimbali hapa jijini dar es salaam.


      Akizungumza kwa kujiamini mkurugenzi huyo alisema kwamba huu ni mpango kazi ambao alikuwa ameuplani muda mrefu sana ili kuwaongezea kipato wasanii wake kabla ya kuingia kambini na kutengeneza albam ingine ya bendi hiyo, alizitaja show hizo sambamba na kumbi zake kuwa ni:-



                     1.Jumatano- Temeke executive lodge
                     2.Alhamisi- swiss pub mbagala charambe
                     3.Ijumaa- Equator grill mtoni kwa azizi ally
                     4.Jumamosi- Smart park ukonga banana
                     5.Jumapili- Sugar ray kwa sokota.


            Hizi ndizo show tano maridadi kabisa za bendi hii ya G five modern taarab yenye maskani yake mtoni kwa azizi ally jijini dar es salaam, uongozi mzima wa mtandao huu unapenda kuchukuwa nafasi hii kuupongeza uongozi mzima wa G five modern taarab kwa utendaji mzuri wa kazi zake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni