TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 1 Aprili 2016

DJ SHUSHU MKONGWE WA MUZIKI WA USWAHILINI "SINGELI" ALIEAMUA KURUDI KATIKA GEMU KWA KASI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


         Unapoamua kuwataja waanzilishi wa muziki huu wa uswahilini almaarufu "singeli" basi jina la Dj shushu ni lazima litakuwa miongoni mwao sambamba na makaveli, msagasumu na khalidy kapaya hawa wote ni watoto wa manzese na mitaa ya mabibo dar es salaam.

DJ SHUSHU MKONGWE WA MUZIKI WA SNGELI.


      Kwa sasa Dj shushu anazisimamia bar zipatazo tatu maeneo ya mbagala akiwa ni Dj wakutumainiwa sana, mtandao huu ulipata bahati ya kuzungumza na mkongwe huyu na kutaka kujua kimya cha muda mrefu alichokuwa nacho ni nini tatizo? nae alianza kwa kucheka na kusema kuwa unajua ndugu mwandishi nilikaa kimya ili kusoma hii gemu ya muziki wetu wa singeli ni nini wadogo zetu wanakosea ili nitakapoibuka tena ni mwendo mdundo hakuna kulemba alizungumza kwa kiswahili cha uswahilini.


    Kwa sasa tayari nina wimbo mpya nimeshaurekodi na upo mikononi muda na wakati wowote utakuwa hewani na mpaka mitandaoni utakuwepo haswa hapa ubuyu wa taarab, maana muziki wetu wa singeli asili yake ni pwani kama ilivyo taarab tu!, wimbo wangu mpya unaitwa "mganga" nimemshirikisha Issa kamongo msanii wa taarab, yeye anasikika katika chorus alafu verse zote namaliza mwenyewe mtu mzima!.

DJ SHUSHU AKIWA KATIKA POZI.

    Wasomaji wa mtandao huu wa ubuyu wa taarab nawaomba tuvute subira na siku mbili hizi nitawawekea wimbo mpya wa Dj shushu ukiwa katika mahadhi ya singeli au ukipenda unaweza kuuita muziki wa uswahilini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni