TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 1 Aprili 2016

OMARY TEGO KUWEKWA "KIKAANGONI" NA WATANGAZAJI WA TAARAB AFRIKA MASHARIKI JUMATATU YA TAREHE 4/4/2016 SAA MOJA USIKU.

NA KAIS MUSSA KAIS.

MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB OMARY TEGO.

            Ile sagment iliyojizolea umaarufu kwa sasa "kikaangoni wiki hii" iliyopo ndani ya group la watangazaji wa taarab afrika mashariki na kati ubuyu wa taarab, wiki ijayo itakuwa na mkurugenzi wa coast modern taarab Omary tego almaarufu "mgodi unaotembea".

 

      Akithibitisha kuwemo ndani ya kipengele hicho Omary tego alisema kuwa amefurahishwa sana na taarifa aliyoipata kuwa watangazaji wamemchagua yeye kuwemo ndani ya group hilo kama mgeni na anaamini atakutana na maswali magumu mno kwakuwa wao wamejiandaa na hajui ni maswali gani atakutana nayo humo!, nimekuwa nikisikia na kusoma katika mitandao juu ya group hili la watangazaji wa taarab na niliamini siku moja nami nitawekwa kikaangoni kama ambavyo taarifa hizi umenifikishia!, mimi nawaambia nimekubali na tuombe mungu jumatatu ifike ili tuwe pamoja humo.

 

      Kikaangoni wiki hii ni sagment iliyopo ndani ya group la whatsap lililosheheni watangazaji wa taarab afrika mashariki na kati yaani tanzania, kenya na uganda, mikoa tofauti ya tanzania watangazaji wamejaa humo, tuvute subira wasomaji wangu ili siku ya jumanne niweze kuwaletea yale yote yaliyo ulizwa na watangazaji pamoja na majibu ya Omary tego yalikuwaje?...TUSUBIRI. Watangzaji ambao bado hamjajiunga humu na wenzenu mnaweza kutumia namba hii 0657-036 328 kuwasiliana na mimi kais mussa kais ili niwaunganishe kwani mnapitwa na mengi sana humu kundini kwakweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni