TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 28 Julai 2017

BI MWANAHAWA ALLY:- KWA SASA HAKUNA TAARAB BALI KUNA TARADANCE ZISIZO NA MUELEKEO!.

Na pambe za taarab

Bi mwanahawa ally au ukipenda muite "jembe gumu" amezungumza na mtandao huu kwa simu tokea visiwani unguja na kushangazwa na khali inavyoendelea katika tasnia hii ya taarab nchini.

Akizungumza kwa msisitizo Bi mwanahawa alisema zamani wakati tunaimba tulikuwa tunafanya hii tasnia kwa mapenzi ya moyoni lakini kwa sasa hali ile imepotea kabisa hakuna tena mapenzi kila kitu pesa na taarab imepotea na imezaliwa hiyo taradance yao masebene kwa kwenda mbele muziki unakimbia utasema treni ya kigoma loooh!, wanapotosha vizazi vya sasa kwa maana ule uhalisi wa taarab hawaupati kabisa.

Hata mimi ukiniona narekodi nakuwa sina jinsi khali ngumu ya maisha nafanya ili nipate pesa lakini nafsi yangu hailidhiki kabisa kabisa. Utakuta wananilazimisha eti Bi mwana jitingishe kidogo wakati wa kuimba, nawajibu siwezi mambo mimi mambo yenu, taarab haswa ikiimbwa unatakiwa ucheze kwa kujitingisha kidogo sio kama wafanyavyo wao mtu anacheza mpaka poda yote inatoka usoni mmmh! siwezi alimaliza kwa kusema.

Bi mwanahawa ally kwa sasa yupo unguja ila jumatatu atakuwa jijini dar kwa mwaliko maalum wa east African melody pale lango la jiji magomeni na jumanne atakuwa na zanzibar stars katika ukumbi wa DDC kariakoo hapa hapa jijini dar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni